Msajili aipa CHADEMA mpaka Jumatatu kupeleka ratiba ya Mkutano Mkuu wa kuchagua Viongozi wao

mawaridi

Member
Aug 30, 2015
47
123
Msajili wa vyama vya siasa aiandikia barua Chadema kupeleka ratiba ya mkutano mkuu wao wa kuchagua viongozi wao

=====

Msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania amekiandikia barua Chadema kukitaka kuwasilisha ratiba ya mkutano mkuu wa kuchagua viongozi wa kitaifa wa chama hicho kabla ya Novemba 11, 2019.

Dar es Salaam. Msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania amekiandikia barua Chadema kukitaka kuwasilisha ratiba ya mkutano mkuu wa kuchagua viongozi wa kitaifa wa chama hicho kabla ya Novemba 11, 2019.

Barua hiyo imetolewa leo Jumatano Novemba 6, 2019 na naibu msajili wa vyama vya siasa, Sisty Nyahoza kwa niaba ya msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi.

Oktoba Mosi, 2019 chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania kiliandikiwa barua na ofisi hiyo wajieleze kwanini wasichukuliwe hatua kwa madai ya kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa kwa kuchelewa kufanya uchaguzi mkuu wa chama hicho.

Chama hicho kilijibu barua hiyo ya msajili kwa hoja sita.

Katika barua hiyo msajili amesema lengo la kutaka maelezo hayo ni kurahisisha ofisi ya msajili kutekeleza majukumu yake.

“Pamoja na mambo mengine, ratiba hiyo ionyeshe tarehe ya kutoa fomu za kugombea kwa wanachama wenye nia ya kugombea, tarehe ya uteuzi wa wagombea na uchaguzi.”

“Taarifa hiyo iwasilishwe ofisi ya msajili siyo zaidi ya Novemba 11 2019 saa 9:30 alasiri,” inaeleza sehemu ya barua hiyo.

Nyahoza alipoulizwa kuhusu barua hiyo amesema imetolewa na ofisi ya msajili, kwamba ni mwendelezo wa barua ya Oktoba Mosi, 2019.

Katibu mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji amelieleza Mwananchi kuwa hajapata barua hiyo, “nipo katika kikao sijaiona barua yenye maudhui hayo.”

Kifungu cha 4 (5) (b) cha Sheria ya Vyama vya Siasa sura ya 258 (RE.2019) kinaipa ofisi hiyo mamlaka ya kufatilia uchaguzi na uteuzi wa viongozi wa vyama vya siasa ili kuhakikisha unafanyika kwa mujibu wa sheria hiyo, katiba na kanuni za chama husika.

IMG_20191106_153219_868.jpeg


2C1B3959-02B4-4EEF-9080-9726CAD037FB.jpeg
 
Hapa ni mwendo wa kumlaumu msajili tu matatizo mengine ni yakujitakia uchaguzi wa ndani ni jambo dogo tu si lazima mpaka ulazimishwe hii ni aibu mbele jamii CCM,ACT,CHADEMA wote waganga njaa hakuna hata mwenye afadhali.
 
Msajili kamiss soda za CHADEMA nini, maana kwa sheria mpya lazima aalikwe kwenye mkutano ahakikishe wajumbe na washiriki wote. Wale walokuwa mchana nzi usiku mbu wanashida awamu hii msajili akiwakuta CHADEMA asiwakute ccm.
 
Hivi huyu msajili yukoje??

Amekomaa kuhakikisha uchaguzi ndani ya Chadema unafanyika, wakati anajifanya "kipofu" na kutoona uchafuzi mkubwa ndani ya uchaguzi wa serikali za mitaa, unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, ambapo uongozi wa juu wa CCM, umetoa "blessings" zao kwa huu uchafuzi wa hali ya juu, ambao haujawahi tokea toka nchi hii ipate Uhuru wake toka kwa mkoloni mwaka 1961, ambapo CCM imejitangazia kuwa imeshinda kwa kishindo kwa wagombea wake kupita bila kupingwa katika sehemu kubwa ya nchi
 
Chadema kwanini munapenda kutafutwa tafutwa... ni kama sasa upinzani hamuna kujua siasa ila mupo na kudekadeka.. kutafuta huruma.. na tayari mumechokwa mbaya.. munaboa sana na upinzani KOKO
 
Kweli wamejipanga. Baada ya kusikia kuna mkutano wa kamati kuu jana basi wameamua wawavurugie kabisa mpaka wasahau kukata rufani. Basi wawaandikie barua ya kuwafuta kabisa.
Mkuu Mromboo, hivi woga wa kufanya uchaguzi unatoka wapi? Hii ndio demokrasia Chadema wanayoipigania? Wakiingia madarakani (sijui kama itatokea anyway) si hata chaguzi watahairisha na kuwa madikteta zaidi ya Hitler?
 
mawaridi,
Msajili anangaika na vitu visivyo na maana na kuacha vitu vya msingi.

-Anaangaika na uchaguzi wa chadema wakati hakuna mwanachama aliyelalamika hata mmoja kuhusu uenyekiti wa mbowe.

-Wapinzani wote wanalalamika kunyimwa haki yao ya kufanya mikutano,wanaibiwa kura kwa figifigisu,wakurugenzi wanatangaza mshindi ambaye kazidiwa kura na wa upinzani,majina yanakatwa pasipo sababu za msingi....Baada ya kuangaikia haya malalamiko ya msingi unaenda kufatilia vitu ambayo havina mashiko yeyote.
 
Afadhali msajili kaingiliw Kati .Mbowe yuko.kimya tu anataka kustukiza uchaguzi watu wasipaye nafasi kujiandaa uchaguzi.mkuu wa Chadema.

Watoe ratiba upesi
 
Kwa hili msajili kakosea timing, huenda Ni kweli chadema wana makosa, kwa sasa issue Ni uchaguzi Wa serikali za mitaa.Alipaswa kusubiri kwanza.Huyu msajili Ni tatizo..
 
Mwambie atoe tamko na huwo upumbavu anaoutolea baraka wa uchaguzi wa serial za mitaa.

Huko haoni?
Afadhali msajili kaingiliw Kati .Mbowe yuko.kimya tu anataka kustukiza uchaguzi watu wasipaye nafasi kujiandaa uchaguzi.mkuu wa Chadema.

Watoe ratiba upesi
 
Mwambie atoe tamko na huwo upumbavu anaoutolea baraka wa uchaguzi wa serial za mitaa.

Huko haoni?
Msajili wa vyama vya siasa sio kazi yake kusiimamia chaguzi za kugombea vyeo vya kisetikali .Chaguzi za kisetikali Ziko chini ya tume ya uchaguzi sio msajili wa vyama vya siasa.Msajili wa vyama vya siasa abahusika na chaguzi za vyama tu.Pelekeni ratiba kwake.
 
Msajili wa vyama vya siasa sio kazi yake kusiimamia chaguzi za kugombea vyeo vya kisetikali .Chaguzi za kisetikali Ziko chini ya tume ya uchaguzi sio msajili wa vyama vya siasa.Msajili wa vyama vya siasa abahusika na chaguzi za vyama tu.Pelekeni ratiba kwake.
Kwa nini Leo?Huyu msajili huenda anatumika sio bure.kwa nini asingesubiri?
 
Back
Top Bottom