Msaidizi wa askofu, RC wakemea udini.

Status
Not open for further replies.

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,903
1,053
Msaidizi wa askofu, RC wakemea udini.


PostDateIcon.png
Monday, 04 October 2010 06:34
Na Waandishi Wetu, Bukoba

ZIKIWA zimebaki siku 27 kabla ya Watanzania kuwachagua wawakilishi wao kuanzia ngazi ya urais, ubunge na udiwani, viongozi wa dini na serikali wamezidi kuwashukia wagombea wanaotumia udini kuomba kura na wale wanaotazama maisha binafsi ya wagombea kwa madai kuwa si sahihi kwani Watanzania hawatafuti askofu au shehe kuwaongoza.

Akizungumza jana katika ibada iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Rumuli Mjini Bukoba, Msaidizi wa Askofu Jimbo Katoliki la Bukoba, Padri Daudi Mubirigi aliwataka Watanzania kutochagua viongozi kwa misingi ya dini zao badala yake wapime sera na umakini wa wagombea.

Padri Mubirigi aliwataka kutokubali kurubuniwa au kununuliwa na baadhi ya watu, kwani huu ni wakati mwafaka kwao kutochezea kura zao ili wachague viongozi watakao kuwa tayari kusimamia nchi na kutumia ipasavyo rasrimali zilizopo kuondoa kero zinazowakabili Watanzania.

Aliwataka Watanzania kutumia haki yao ya kupiga kura Oktoba 31 mwaka huu kwa kuhakikisha wanawachagua viongozi bora watakaosimamia shughuli mbalimbali za serikali na kuwaletea maendeleo wananchi.

Padri huyo alitumia muda huo kuwaonya baadhi ya wagombea wanaotazama maisha binafsi ya wagombea wenzao, akisema kuwa kama hiyo ikigeuka kuwa agenda basi hakuna mtu atakayesimama salama katika mchakato wa uchaguzi.

Alisema kuwa Watanzania hawatafuti askofu wa kuongoza nchi ambaye anatakiwa atazamwe mwenendo wake, bali wanataka rais atakayesimamia nchi, atakayepambana na ufisadi ili rasrimali zitumike kuwanufaisha wananchi wote na si baadhi ya watu, huku akiongeza kuwa mambo ya kuangalia mgombea ana wanawake au nyumba ngapi hayahusiki katika kumtafuta rais.

Ingawa Padri Mubirigi hakutaja jina la mtu yeyote, lakini katika siku za hivi karibuni tangu kuanza kwa kampeni imeibuliwa hoja juu ya maisha binafsi ya Mgombea Urais wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Willibroad Slaa, akidaiwa kutembea na mke wa mtu ambaye yeye amekuwa akimtambulisha kama mchumba wake, Josephine Mshumbusi.

“Hatutafuti askofu wa kuanza kutazama mwenendo na maisha wake, tunachokitafuta ni
rais atakayewasaidia wananchi kujiletea maendeleo mambo ya kuwa na wake wawili au zaidi hayatuhusu, akipenda wanawake wengi atakufa kwa Ukimwi huko,” alisema padri huyo.

Padri Mubirigi alifafanua kuwa wapo baadhi ya watu wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maneno, katika simu yake wakitaka kutochagua kiongozi fulani kwa sababu ya dini yake.

Wakati huo huo wananchi wa Kagera wametakiwa kuwa makini katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 31 mwaka huu kwa kuwachagua viongozi watakao wasaidia katika kuinua maendeleo ya mkoa wao na kuepukana na wale wanaoeneza siasa za ukabila na udini unaoelekea kukua kwa kasi kwa baadhi ya maeneo mkoani humo.

Rai hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa Kagera, Bw. Mohamed Babu wakati akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa uongozi wa Mkoa wa Mwanza, katika makabidhiano yaliyofanyika Katoro, wilayani Chato, ambao utakimbizwa mkoani hapa kwa siku nane.

"Kwa sasa katika uchaguzi wa mwaka huu, katika mkoa huu kwa baadhi ya maeneo kumeibuka siasa za ukabika na udini, jambo ambalo ni hatari kwa taifa ni jukumu la wananchi kuwa makini katika kuchagua viongozi watakaowasaidia kuinua maendeleo yenu na ya mkoa kiujumla na si ukabila na
udini," alisema Bw. Babu.

Hata hivyo, bila kutaja maeneo hayo ambayo ukabila na udini umeibuka, aliwataka wananchi kuwapuuza wagombea wanaotaka kuchaguliwa kwa kuzingatia udini na ukabila kwa vile vinapingana na sheria ya uchaguzi hata mwongozo wa wananchi.

Katika hatua nyingine Bw. Babu alisema jumla ya vyandarua vyenye viuatilifu vipatavyo 261,721
viligawiwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano na akina mama wajawazito kwa
kipindi cha mwaka 2006 hadi 2010.

Watu wazima waligawiwa vyandarua 560,484 kuanzia Julai 2009 hadi sasa ambapo walengwa walikuwa ni 444,234 lengo lilikuwa ni kupambana na milipuko ya Malaria kutokana na mkoa huo kuwa wa pili kwa mapambano wa ugonjwa huo kwa nchi nzima. Alisema kutokana na hali hiyo vifo vya watoto vimepungua kutoka asilimia 22.8 kwa mwaka 2002 hadi asilimia 13 kwa mwaka
2008.

Mwenge utazindua miradi 88 wenye thamani ya sh.bilioni 7.1 katika wilaya zote
za mkoani Kagera huku asilimia 56 ya miradi hiyo ikiwa ni nguvu za wananchi
wahisani ikiwa ni asilimia 15. Ambapo kwa Wilaya ya Chato umezindua miradi minane
yenye thamani ya sh. Milioni 360.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom