Msaidizi wa Askofu Gwajima atoa Tamko

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
May 2, 2016
559
808
1.jpg


Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, jana walisali bila kuwapo kwa Askofu wao, Josephat Gwajima ambaye anatafutwa na Jeshi la Polisi.
Mara nyingi Jumapili, Gwajima ndiye amekuwa akiongoza ibada katika kanisa hilo lililopo Ubungo Kibo, lakini jana iliongozwa na mchungaji Edward Adriano ambaye hata hivyo, hakueleza chochote kuhusu alipo askofu huyo.

Gwajima anatafutwa na polisi baada ya kusambaa kwa sauti inayosikika kama yake akitaka Rais mstaafu, Jakaya Kikwete afikishwe mahakamani kwa yote yaliyofanyika wakati wa utawala wake.
Jana, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema suala la Askofu Gwajima atalizungumza leo.

Alhamisi iliyopita Polisi walizingira nyumbani kwa Gwajima kwa saa saba, wakitaka kumkamata bila mafanikio.
Kamanda Sirro alisema wanamtafuta askofu huyo ili athibitishe kama maneno yenye uchochezi, yanayosambaa kwenye mitandao ni ya kwake.

Ulinzi kanisani
Ulinzi katika kanisa hilo jana uliimarishwa na vijana waliovaa vizibao vya njano, vilivyoandikwa polisi jamii tii sheria bila shuruti. Idadi ya vijana hao wanaokadiriwa kufika 40, walikuwa wengi kuliko Jumapili nyingine zilizopita.
Licha ya kutokuwapo kwa askofu huyo kanisani hapo, waumini walijaa na wengine kukosa viti huku wengine wakionekana kusimama nje ya kanisa hilo.

Kauli ya Msaidizi wa Gwajima
Msaidizi wa Askofu Gwajima, Yekonia Bihagaze, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, alisema juzi kuwa taratibu, sheria na kanuni zinapaswa kufuatwa kumkamata kiongozi wao.

"Kanisa la Ufufuo Na Uzima ni makini, tulivu na halikurupuki kwenye maamuzi yake. Na nchi haiongozwi mitandaoni, kama serikali inamtaka mtu ziko taratibu, sheria kanuni za kuzifuata," sehemu ya taarifa ya Mchungaji Bihagaze ilisomeka.

"Kwa sasa kila mmoja anaona nchi inapiga hatua kimaendeleo, ni vema wananchi sasa tukaachana na propaganda kama hizi, ni vema tukaweka shabaha yetu moja kushirikiana na Rais tulijenge taifa Letu. Taifa hili si mali ya mtu mmoja, ni mali yetu sote kwa manufaa yetu na vizazi vingine vitavyokuja.

"Adui wa Rais wetu awe adui yetu sote. Siasa zitakuja tu baadaye ila kwa sasa nchi itulie, watu tuchape kazi, tulipe kodi kwa sababu kuna Rais mwenye nia ya kuipeleka mbele.

"Hakuna duniani Taifa linaloweza kuendelea pasipo wananchi kushirikiana bega kwa bega na kiongozi wao."
 
Ajitokeze aonyeshe ujasiri wake na hasa ukizingatia anaongozwa na roho wa Mungu, hatadhurika kwa kuwa aliyokuwa anayasema aliongozwa na roho wa Mungu wake: sasa anajificha nini: sijui kala maharage ya wapi huyu, nilikuwa namheshimu sitamheshimu tena.....
 
Ajitokeze aonyeshe ujasiri wake na hasa ukizingatia anaongozwa na roho wa Mungu, hatadhurika kwa kuwa aliyokuwa anayasema aliongozwa na roho wa Mungu wake: sasa anajificha nini: sijui kala maharage ya wapi huyu, nilikuwa namheshimu sitamheshimu tena, anafungwa pampasi.....
Hivi kujificha si ni sawa na kusema uongo ambao umekatazwa? Yaani mtu upo halafu unasingizia haupo na pia wasaidizi wako kiroho wanasema hawajui ulipo wakati wanajua ulipojificha. Kwa nini viongozi wa dini wafikie kudanganya kuwa hawajui alipo mwenzao ili tu asijedakwa na vyombo vya dola vinavyomtafuta huku wakijua wazi kabisa kwamba kusema uongo wa aina yoyote kumekatazwa kwenye vitabu vitakatifu? Kweli uongo ni dhambi inayotutafuna wengi sana.
 
Ajitokeze aonyeshe ujasiri wake na hasa ukizingatia anaongozwa na roho wa Mungu, hatadhurika kwa kuwa aliyokuwa anayasema aliongozwa na roho wa Mungu wake: sasa anajificha nini: sijui kala maharage ya wapi huyu, nilikuwa namheshimu sitamheshimu tena, anafungwa pampasi.....
Loooh!!!
 
Ajitokeze aonyeshe ujasiri wake na hasa ukizingatia anaongozwa na roho wa Mungu, hatadhurika kwa kuwa aliyokuwa anayasema aliongozwa na roho wa Mungu wake: sasa anajificha nini: sijui kala maharage ya wapi huyu, nilikuwa namheshimu sitamheshimu tena, anafungwa pampasi.....
Teh teh....mkuu hata manabii na mitume walikuwa wanajificha yakiwakuta, sembuse "askofu"!!
 
mtu asiyejambazi anaenda kukamatwa na defender kibao hii ndo TZ
Mmh! Ndugu,ukifanya uchochezi ni jambo kubwa sana kuliko unavyofikili.tunaipenda Tanzania yetu na hatutaki kuweka tofauti ya kimaelewano kati yetu wananchi na viongozi wetu,au kati ya uongozi uliopo na uliopita,unaposema hayo sehemu ya ibada unatengeneza chuki wa waumini ambao ni wananchi.MUNGU atusaidie sana
 
Back
Top Bottom