Msaidieni huyu jamaa.... anaumwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaidieni huyu jamaa.... anaumwa

Discussion in 'JF Doctor' started by kipusy, May 10, 2010.

 1. kipusy

  kipusy JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 540
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60
  JF DOCTORS msaada wenu unahitajika sana, Kuna jamaa yangu mmoja anasumbuliwa na vitu viwili
  1) Huwa anawashwa bila sababu, hana upele, ila akiwa anajikuna vile vipele vya kuku vinatokeza vingi. baadae muwasho unapoa vipele vinatoweka. anamuda sasa tangu aanze kupata matatizo hayo.

  2) Alianza kukohoa tangu Mwezi wa pili trh 10, mpaka leo hajapona na huwa akihema kwa nguvu mapafo au kwenye koo kuna unguruma, ametumia dawa zote muhimu za kawaida za kifua lakini bado hazijasaidia.

  NASUBIRI MAONI YENU WANA JF
   
 2. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  1.MWANAUME AU MWANAMKE? 2.UMRI 3.YUPO MKOA GANI 3.SEHEMU HASA YA MUWASHO [MAUNGIO.MWILI MZIMA AU WAPI?]4.KIFUA KILIANZA SAMBAMBA NA KIKOHOZI AU?KIPI KILITANGULIA5. VIPELE VYA KUKU?[UNAMAANANISHA NINI,SEHEMU GANI YA KUKU YENYE HUO MFANO e.x.mdomo,mguu?]6.kwao kuna wagonjwa wa kifua ex.pumu n.k?7.NI AKIWA KATIKA MAZINGIRA GANI NDIO TATIZO LINAANZA[NYUMBANI KAZINI,SHAMBANI],JE MUWASHO UKIANZA HUAMBATANA NA MAFUA[CHAFYA,KUWASHA MACHO NA MACHOZI AU KIOH ZI?].
  Dawa gani alitumia?
   
 3. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280

  Huo muwasho wa mwili nahisi kama ni Allergy ya sabuni ya kuogea au misosi anayokula au mafuta/lotion anayotumia au manyoya ya paka,mbwa nk.
   
 4. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ashaenda Hospitali kuonana na madaktari?Mie nadhani hana haja ya kuogopa hospitali.Litakuwa ni jambo la busara zaidi kwenda kwenye vipimo kuliko kuomba msaada wa ushauri hapa kutokana na hizo dalili za ugonjwa.
   
 5. kipusy

  kipusy JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 540
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60

  Huyu ni kidume, umri miaka 32, hupo hapa dar kimasomo, huwa anawashwa mwili mzima, Kikohozi kinaendelea mpaka leo, na anapumua kwa shida inapelekea kikohozi, vipele vya kuku kumaaa..nisha vipele kama vile vipele pale mtu unapokua na baridi, Kwao hakuna wagonjwa wa punu wala vfua, Muwasho hutokea pale anakua anataka kulala au ametoka kazini anavua nguo, na anapokua amemaliza kuoga. Huu muwasho wake hua hauambatani na kifua chafya, mafua, kikohozi wala chafya ingawa huwa anakohoa sana kama nilivyoeleza hapo juu lakini hajui kama muwasho huo unaambatana na kifua na kukohoa,

  Dawa alizotumia ni Vidonge flani vidogo vya allegy jina siliojui alipewa na daktari kwa ajili ya muwasho,
  Kifua alikunywa Ammoxlin na dawa nyingine za maji (ZECUF)
   
 6. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  plz go and see the doctors asap
   
 7. MLATIE

  MLATIE Senior Member

  #7
  May 11, 2010
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 174
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Aende hospitali wakampime allergy test itamsaidia sana aache kumeza dawa bila ya kuwa na mpangilio mara nyingi zinzzidisha ugonjwa na kuufanya uwe sugu zaidi.Namshauri aende hospitali kwa kupata matokeo mazuri zaidi
   
 8. ismase

  ismase Senior Member

  #8
  May 11, 2010
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Asisahau na ushauri nasaha
   
 9. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  .kuwashwa kwa jamaa yako bila mlipuko wa ngozi naweza kuuweka katika kundi la GENERALIZED PRURITUS [intense itching of the skin without eruption].PRURITUS huwa ni dalili [SYMPTOM] inayowakilisha ugonjwa, hivyo muwasho huo huhesabiwa kama moja ya dalili kiashirio cha ugonjwa Fulani.Muwasho kama wako kwa jinsi ulivyouelezea unaweza kudondokea katika makundi mawali[1] Unaosababishwa na mazingira ya nje [surface causes].maadamu mazingira ya allergy umeyakataa kimaelezo na kitiba,..hali ya SCABIES, [also known as sarcoptic acariasis ] tunaweza kuiizingatia zaidi kwenye suala la ugonjwa wako.[a]Alianza kukohowa tangu mwezi wa pili kikohozi chake ni severe,sababu kinaambatana na mikoromo pamoja na kupumua kwa shida,.hiki kikohozi cha muda mrefu ni pelekeo la kushuka kinga mwilini,hii ni moja ya vigezo vya kushambuliwa na wadudu hawa.b]Wadudu hawa huanza kuonyesha dalili kuanzia wiki nne mpaka sita,baada ya kuingia kwenye ngozi.Dalili zake ni muwasho,na mabadiliko ya ngozi kwa baadhi ya sehemu kutengeneza mistari ulionyanyuka[burrows],na wakati mwingine mwisho wa huo muinuko huonekana kama kamuumuko kama ka chunusi [bump]. NEXT
   
 10. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mara nyingi miinuko hiyo[burrows] huonekana zaidi kwenye vidole au katikati yake.,juu ya viganja,katika maungio ya mikono [ elbow ] ,kwenye maumbile ya [male genitalia] kwenye kiuno sehemu ya mzunguko wa mkanda na chini ya ******.Michirizi ya kwenye ngozi sababu ya kujikuna.Kama hizo barrows zitakuwa sehemu za wazi kama mikono na kwingine ni rahisi kuziona kwa kutumia lenzi ,lakini kama ni sehemu zilizojificha, huwa siyo rahisi kuzijua wala kuziona.c] Muwasho wa scabies hutokea kuwa mbaya zaidi mara baada ya kuoga,zaidi maji ya moto ,lakini wakati mwingine na ya baridi pia,.kama ilivyo kwa rafiki yako.[d] Hali ya muwasho wa wadudu hawa huongezeka zadi kipindi cha usiku.[,ambacho wote huwa tunalala,.na tunakuwa tumetoka kazini]MATIBABU;Ni baada ya kugundua uwepo wa burrows, Hivyo aende kwa daktari wa ngozi akaangaliwe vizuri.Na pia apimwe vizuri hicho kifua na Xray isomwe vizuri na Mwenye uelewa.,huo ni muda mrefu toka aanze kukohoa.
  NEXT
   
 11. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #11
  May 11, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ***=CHINI YA MAKALIO,II; Katika kundi hili la pili PRURITUS inaweza kusababishwa sababu za ndani [a]magonjwa ya ini kushindwa kufanya kazi kwa figo [c]upungufu wa madini ya chuma [d]kisukari [e]thyroid [f]Cancer .Mfano kama HodgkinÂ’s disease, ambapo muwasho hutokea mapema,zaidi kabla ya tatizo,na muwasho wake huenda bila mabadiliko yoyote kwa upande wa ngozi. NENDA HOSPITALI YA RUFAA,AANZIE KWA DAKTARI WA NGOZI KWANZA,KUWASHA HAKUWEZI KUPONA BILA KUTIBU UGONJWA ILIOUSABABISHA
   
 12. b

  bwanashamba Senior Member

  #12
  May 11, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  plz go hospital and see Doctor/na ukweleze ABCD up to
  Z THEN UTAPATA SULUISHO
   
 13. J

  Jafar JF-Expert Member

  #13
  May 12, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Just tell him to attend OPD, c the doctor and will be cured. Dont waste time, attend to hospital now (today).
  Is he out of reach of any hopsital?
   
 14. kipusy

  kipusy JF-Expert Member

  #14
  May 12, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 540
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60
  nimekupata mzee
   
 15. kipusy

  kipusy JF-Expert Member

  #15
  May 12, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 540
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60


  Hapo sijakupata mwanzo wa sentence, je unaweza kuwambukiza mtu kwa njia ya kujamiiana?
   
 16. kipusy

  kipusy JF-Expert Member

  #16
  May 12, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 540
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60
   
 17. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #17
  May 12, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Inaweza kuwa egzma ila mshauri aende hosp
   
 18. kipusy

  kipusy JF-Expert Member

  #18
  May 12, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 540
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60
  hapo kwenye colour text weka wazi, uwelewa tunatofautiana, hapa unaokoa maisha ya mtu haina haja ya kuficha neno.
   
 19. kipusy

  kipusy JF-Expert Member

  #19
  May 12, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 540
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60
  Kama kuna mtu anajua wapi anaweza kupata matibabu ya uhakika naomba aelekeze, Ikiwezekana na Jina la Doctor
   
 20. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #20
  May 12, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Niliwahi sikia maeneo ya tegeta huko kuna hospitali moja nzuri wataalam wa ngozi jaribu!
   
Loading...