Msafara wa Viongozi ni Usalama au fahari? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msafara wa Viongozi ni Usalama au fahari?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiroroma, Mar 2, 2010.

 1. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2010
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 369
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Asubuhi ya leo nikiwa mbele ya kituo cha Polisi Salendar Bridge ulipita msafara wa kiongozi mmoja wa juu serikalini anaenda zake ofisini ulikuwa msusururu wa magari ya kifahari yapatayo sita na pikipiki,Sasa nikajiuliza msafara ni kwa ajili ya wanausalama tuu au ni ufahari fulani?Wana JF nisaidieni hapa.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Hujauona msafara wa JK siku hizi...Full Obamization...umeongezwa vimbwanga vya marais wa Amerika, utasema ni bonge la nchi tajiri..kumbe ni maigizo ya utoto tu...One Man Show Thing!

  Magari kibao nani ana mpango wa kuwaua nyie?

  Masikini akipata.......!! mi nawatazamaga hawa wakuu weee, sielewi kitu!
   
 3. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2010
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  By the way mimi pia huwa nakutana na kigogo mwingine msafara wake si mrefu ni magari mawili meusi ya kifahari (yanavutia!) sidhani kama haya yatakuwa ya kodi zetu...:rolleyes: huwa yanapita kwa mwendo kasi...huyo tena ni nani? Hivi wangapi wanatakiwa kupitishwa? Prezida, PM, fomer Prezidents, Former ? Usalama wa taifa? Nani tena maana mwishoe kutakuwa na foleni za misafara halafu wengine tutabidi kukaa home!
   
 4. A

  Adili JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2010
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 2,283
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  Ni ufahari na vishindo.
   
 5. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 276
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Tatizo hujawa specific,ni kiongozi yupi,magari ya kifahari yapi(maana kila mtu ana vipimo vyake vya magari ya kifahari).Kwa viongozi kama Rais,Makamu wake au waziri mkuu hizo ni taratibu za kawaida kabisa za ulinzi.Kama unakumbuka tulivyompoteza Sokoine,lawama zilienda kwa wanausalama,sababu ya Escort chache zilizopelekea gari ya waziri mkuu kugonga gari ambayo haikuwa kwenye msafara.
   
 6. dorin

  dorin Senior Member

  #6
  Mar 2, 2010
  Joined: Jan 29, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Duh hapa ningempata wa kunipa maelezo kamili ningefurahia sana
  Mi naonaga kama kero. Kuna siku Tulisimamishwa ile kona ya kutokea Ikulu
  Kwa muda wa nusu saa ndo msafara unapita. Nilijiuliza maswali Mengia sana
  yasiyokua na majibu.
   
 7. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 276
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Hakuna maelezo ya maana zaidi ya uzembe unaosababishwa,ama na mawasiliano mabaya kati ya Usalama wa taifa na police,lakini nachoelewa ratiba ya kiongozi mkubwa hutolewa mapema kwa Rpc wa eneo husika,sasa utakuta uoga wa askari wa usalama barabarani wanasimamisha magari mapema wasiharibikiwe na kazi,na kumbuka amri ya kusafisha njia inatoka kwa RTO(Region Traffic Officer) kupitia Radiocall,ambaye gari yake inakuwa mbele kwenye msafara ikisafisha njia.Au unaweza kuta ni sababu za kiusalama kwa siku ile.
   
 8. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,776
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Ni upotezu wa mafuta tuu kama siku ikifika imefika no way out!
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 42,002
  Likes Received: 37,300
  Trophy Points: 280
  Kwani hujui kuwa huu ni uongozi wa mbwembwe na ubitozi?
   
 10. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #10
  Mar 2, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 462
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Msafara ndio maana ya Urais. Kama wakisema gombeeni urais, lakini hakutakuwa na misafara, wala kutandikiwa mazulia mekundu majuu, nani atagombea?

  The rest are just details...
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...