Msafara wa viongozi kufunga barabara

chifu77

JF-Expert Member
Aug 2, 2014
902
595
Habari wakuu.
Hapa simlengi mkulu wa nchi, naibu wake na PM.

Namaanisha mawaziri na manaibu wao. Wanapokuwa katika majukumu yao unakuta baadhi ya barabara zimefungwa na kusababisha foleni na usumbufu kwa raia. Hivi ni sheria ipi inayoruhusu kufunga barabara tena kwa masaa 2 au 3 ili kusubiri wapite? Unakuta sisi wengine tunatoka Vijijini, tumekuja mkoani na tunakimbizana na ratiba za mabasi ya abiria. tena ukiulizia unaambiwa Mheshimiwa anamalizia kikao kisha atoke au bado anakula, lakini huku barabara zimeshafungwa.

Nafahamu kuwa katika 'Basic Traffic Offences' obstruction of VIP motorcade ni kosa ( s. 43) ambalo unaweza kutozwa faini 30,000 - 50,000 au kwenda jela miezi 6 na isizidi miaka 2. Au vyote kwa pamoja.

Sasa ni sheria ipi inayosema barabara ifungwe, mpaka apite? Kwa nini hata wasinge time ule mda wanatoka ndo wafunge angalau dakika 10 zinatosha?

Wenzetu mnaoishi ughaibuni ambao wanajali mda, wao wanafanyaje katika hili?
 
Back
Top Bottom