Sio kweli. Wala Marekani haijawahi kuficha aina ya Silaha inazozipeleka nchini Ukraine tangu Mwanzoni wa uvamizi wa Urusi Kama kweli umefuatilia mgogoro huu.
Msafara wa Magari ya kivita wa Urusi uliokuwa na urefu wa 64km ilikuwa mwezi wa 3. Marekani ilitangaza kutuma mifumo 4 ya HIMARS tarehe 16 Julai. Kwahiyo HIMARS hazikuhusika katika kuusambaratisha msafara huo wa Urusi.
Kama HIMARS zingelikuwepo Mwanzoni wa uvamizi basi Urusi isingeliweza kabisa kuyateka maeneo Yale kwa haraka Sana. Ukicheki Ramani ya Ukraine utagundua kwamba,Tangu Majeshi ya Ukraine yapatiwe Mifumo ya HIMARS basi Urusi haijateka mji wowote ule. Miji ilitekwa kwa haraka kabla ya ujio wa HIMARS.