Msafara wa Maalim Seif wapata ajali Mwanza

Msafara wa Maalim Seif wapata ajali Mwanza

Mandla Jr.

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Posts
3,098
Reaction score
631
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad umepata Ajali mbaya Mkoani Mwanza na kupelekea Viongozi mbalimbali wa Chama hicho kuwa na hali mbaya.

Vilevile Mkurugenzi huyo wa Habari wa Chama hicho alisema kwa sasa Majeruhi hawo wamekimbizwa kwenye Hospitali ya Bugando kupatiwa matibabu na hali yao inaendelea vizuri isipokuwa Katibu chama cha Cuf kutoka Wilaya ya Nyamagana Rehema Mwenda hali yake sio Nzuri kutokana na kupoteza Fahamu
Naibu Mkurugenzi wa Habari kutoka Chama cha Wananchi CUF bwana Kambaya alithibitisha kutokea kwa Ajali hiyo na kusema Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Maalim na Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) Seif Sharif Hamad ajadhurika na yuko salama bali waliodhurika na Ajali hiyo ni viongozi wa chama hicho,

“Ni kweli Msafara wa Makamu wa rais na Katibu mkuu Taifa umepata ajali ila yeye yuko salama,lakini viongozi wetu wa chama akiwemo katibu wa Chama cha Wananchi CUF Wilaya ya Nyamagana Be Rehema Mwenda Pamoja na Mkuu wa Kitengo cha cha Habari wa chama Chetu wilaya ya nyamagana Hassan Shido ndio wamepata majeraha kutokana na Ajali hiyo,”alisema Kambaya.

Kambaya alizidi kusema Ajali imetokana na Dereva wa Gari aina Scania kwenda kuligonga Gari lilokuwa limewabeka viongozi hao,ambapo gari hilo lilikuwa la nne kutoka gari lililombeba Maalim Seif kwenye msafara huo.

10383026_365653033585072_97665310246320442_n.jpg

10649576_365653036918405_2710866997486703669_n.jpg

Mkurugenzi wa habari wilaya'na MH SHIDO Ambae ni mwenyekiti wa serikal ya mtaa uliyopo kata ya miringo,wameumia vibaya wamelazwa hospitali ya BUGANDO
 
Poeni wapiganaji, tunawaombea kwa mungu mupone ili muendelee na kazi nzuri ya kuendeleza taifa
 
Ninavyojua mimi Makamu wa Rais ni kiongozi Mkubwa sana ina maana polisi au serikali ilikuwa haijui kuwa Msafara wa Makamu wa Rais SUK atapita hapo! Mbona barabara zinafungwa Mkuu tu wa Mkoa anapopita eneo flani na msafara wake kusindikizwa na vingora mbele na Nyuma? Jamani Tuzindukeni sasa Watanzania CCM inatupeleka kuzimu kwa hizi double standard zao!
 
Acha tu wanamzarau sanaa niliona siku moja ubungo mataa msafara wake ukipiga honi upishwe ukitokea ubungo plaza

ipo siku yataisha tuuu, poleni wote.
 
Ninavyojua mimi Makamu wa Rais ni kiongozi Mkubwa sana ina maana polisi au serikali ilikuwa haijui kuwa Msafara wa Makamu wa Rais SUK atapita hapo! Mbona barabara zinafungwa Mkuu tu wa Mkoa anapopita eneo flani na msafara wake kusindikizwa na vingora mbele na Nyuma? Jamani Tuzindukeni sasa Watanzania CCM inatupeleka kuzimu kwa hizi double standard zao!

Sasa mtu anataka zanzibar iliyo huru ili apumue, unategemea nani atampa huo ulinzi?
 
Pole zao! Kwa hiyo Maalim Seif yupo SAWA SAWAAAAAAA.

Hahahaha umenikumbusha hako ka msemo ka maalim pindi anapokuaga anawahutubia boko haram.
Utasikia vibwagizo... mpo sawa sawaaaaaaah???
Tetetete.
 
Hivi Julius mtatiro ni nani cuf siku hizi mbona hasikiki?
 
MAALIM SEIF APATA AJALI: Makamu wa 1 wa Rais Z'bar, Maalim Seif S. Hamad anusurika kifo leo mchana baada ya msafara wake kupata ajali eneo la Misungwi, Mwanza.
 
Back
Top Bottom