Msaada yahoo mail

OMGHAKA

Member
Joined
Aug 15, 2011
Posts
97
Reaction score
24
Wadau, nimekuwa nikitumia Yahoo Mail kwa muda lakini hapa karibuni walilazimisha ku-up date e-mail yangu na tangu hapo ziwezi tena ku-attach files kwenye e-mail.
Kama kuna jinsi naweza fanya naomba msaada wanajamvi
 
unataka kuattach document aina gani na ya size gani???
 
Hilo tatizo nililipata zaidi ya miezi miwili kiasi kwamba imenibidi nihamie Gmail hata hivyo inategemea na network maana kwene simu naweza ku-access bila shida na pia kwa baadhi ya maeneo haina shida, nilijaribu ku-go back to the older version ikagoma pia. Siwezi hata kusoma mails achilia mbali ku-attach na ku-download. nimeripoti but still no response na sasa ni kila mtu hapa ofisini mwenye account yahoo ana face the same problem. Sijui kwa kweli labda tusikilize wajumbe wengine.
 

the same problem!!!tabu tupu.siwezi kuchat harakaharaka-wananiambia sijajiunga na yahoo messenger-ili mradi haiko sawa
 
unataka kuattach document aina gani na ya size gani???

Doc 67kb imegoma, xls, 45 kb imegoma, pdf 87kb imegoma, ziped folder 37kb imegoma...aaah!!!
 
tena gmail wanakupa storage ya 7+GB na you can send sms free na mahuduma kibao, na wana-group mails zinazotoka kwa adress moja so ni rahisi sana kujua mazungumzo yako na watu wengine and so much, siwafagilii ila wako vizuri sana
bora nianze na Gmail.
 
Mimi nikijaribu kulog in na computer inakataa. Na simu inakubali. Nifanyaje maana siwezi kusoma emails zenye attachments kwa simu.
 
Wadau, nimekuwa nikitumia Yahoo Mail kwa muda lakini hapa karibuni walilazimisha ku-up date e-mail yangu na tangu hapo ziwezi tena ku-attach files kwenye e-mail.
Kama kuna jinsi naweza fanya naomba msaada wanajamvi

Tatizo hilo limejitokeza mara hawa jamaa walipokuja na version mpya wanayoiita Yahoo Beta. na kwa bahati mbaya wanakuwa wanalazimisha kila mtu a swtch toka classic kwenda kule. Kuna baadhi ya watu wanaifurahia Yahoo beta. mimi kama wewe haikuwa friendly kabisa.

Nilichofanya ni ku uncheck Java sript (mie natumia browser ya mozilla - unaenda Tools - Options - Content - kibox chenye tick kimeandikwa Enable java script - wewe ondoa hiyo tick wakati wote ukiwa kwenye hiyo Yahoo Beta. Re start computer then omba Yahoo - itakuja Classic. Ikishakuja yahoo classic nenda karudishe tick kwenye kibox cha Enable Java script.

hata hivyo inabidi uwe macho sana kila wakati watakurubuni urudi kwenye beta!!. Wengi hawaipendi nimesoma forums kadhaa - pengine magwiji wa software huenda wanaimudu hii Yahoo mpya. But am comfortable with my yahoo Classic.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…