Kuna application kaweka kwenye simu yako inayodukua mawasiliano na hizi application huwa ni ngumu kuziona sababu huwa zinafichwa na ukizitafuta kwenye setting huwezi kuziona maana huchukua majina ya default app zilizomo kwenye simu. Utakuta imeandikwa wifi, bluetooth au majina mengine kwahiyo ni vigumu kugundua. Hapo inabidi urestore simu yako kwa iTune yaani uanze upya. Kuna tutorial nyingi youtube zinazoelezea Jinsi ya kurestore simu ya iPhone. Ila kama umesahau email na password za iCloud usifanye hivyo maana hutaweza kuitumia tena simu yako. Kama utashindwa kurestore hakikisha mawasiliano yako ya muhimu unayafanyia kwenye simu ndogo ya button tena hizi ambazo zinatumia pin ndogo au kubwa.
Pole sana. Ila mwambie shemeji aache wivu.