Justine Marack
JF-Expert Member
- Jul 31, 2014
- 606
- 1,675
Nimeagiza gari toka Japan na baada ya kuanza biashara nimepata changamoto ya matumizi ya mafuta. Gari ni Toyota hiace, Engine ni 2RZ na ni automatic. Gari inatumia lita moja ya mafuta ya petrol kwa kilomita 3.7 na ilitakiwa angalau kutumia kwa wastani wa kilomita 7 kwa lita. Kama unajua lolote nijuze kwa kuwa newaendea mafundi kadhaa kila mmoja kasema yake. 1. Plague 2.Wiring 3. Sensor 4. .... hata sikumuelewa vema. Wadau wenzau wanasema hata wao walikua na hiyo hali ila kila mmoja inaonekana alisolve kwa njia tofauti yaani hakuna njia iliyo common kwa wote. Nikipata mawazo yenu nita mweleza fundi aliye karibu nami ili alifanyie kazi. Tafadhali mimi sipo dar so sina namna ya kuleta gari ofisini kwa mtu wa dar, nipo Mikoani so msaada wako wa mawzo nitasema na fundi wa huku. Nisaidieni