Msaada wenu wa Utaalamu

Justine Marack

JF-Expert Member
Jul 31, 2014
534
1,466
Nimeagiza gari toka Japan na baada ya kuanza biashara nimepata changamoto ya matumizi ya mafuta. Gari ni Toyota hiace, Engine ni 2RZ na ni automatic. Gari inatumia lita moja ya mafuta ya petrol kwa kilomita 3.7 na ilitakiwa angalau kutumia kwa wastani wa kilomita 7 kwa lita. Kama unajua lolote nijuze kwa kuwa newaendea mafundi kadhaa kila mmoja kasema yake. 1. Plague 2.Wiring 3. Sensor 4. .... hata sikumuelewa vema. Wadau wenzau wanasema hata wao walikua na hiyo hali ila kila mmoja inaonekana alisolve kwa njia tofauti yaani hakuna njia iliyo common kwa wote. Nikipata mawazo yenu nita mweleza fundi aliye karibu nami ili alifanyie kazi. Tafadhali mimi sipo dar so sina namna ya kuleta gari ofisini kwa mtu wa dar, nipo Mikoani so msaada wako wa mawzo nitasema na fundi wa huku. Nisaidieni
 
fanya service mkuu ya kawaida cheki plug nunua nyingine usiweke bora plug kwa kuwa unaweza ingia google search utapata aina ya plug zinazotakiwa kwenye 2rz


fungua distributer fanyia usafi kuanzia cap na rotor yake.

njoo kwenye mafuta safisha fuel filter ukiona chafu sana fungua na nozel zisafishe

fungua idle sensor isafishe pia

check air clener kama limechoka nunua jingine.

hapo hapo kwenye air clener kuna sensor MAF sensor hiyo ndio ugonjwa mkubwa unaoweza kusababisha gari kula mafuta je ni nzima ??


swali vipi hali ya gari unapoliendesha lipo kawaida jepesi??

pili vipi moshi wa gari upo katika hali gani?? ni wa aina gani?? mweusi ??

kwa kuwa gari umeagiza yapaswa isitoe moshi kabisa coz bado ipo kwenye hali nzuri.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom