milangomitatu
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 1,469
- 1,167
Tenga kila mwezi tzs 42,000 kutoka katika mshahara wako.Nimeanza kazi na nimelipia nyumba laki 2 na nusu kwa miezi 6 sasa kichwa kinauma ikiisha hyo miezi 6 itakuwaje?naomba msaada kwa wazoefu hela za miezi 6 mnatoaga wapi? Una save kwenye mshahara au unakopa? Natumai ntapata jibu sahihi Asanteni
Asante sana kwa ushauriTenga kila mwezi tzs 42,000 kutoka katika mshahara wako.
Hicho kiasi kihifadhi kwenye M-Power (mfano).
Baada ya miezi sita utakuwa na kiasi kinachotakiwa kulipia kodi ya nyumba kwa miezi sita mingine.
Zoezi la kutunza fedha liwe endelevu.
nenda PSPF wakupe MKOPO WA KUANZIA MAISHA
Mkopo wa Jipange Kimaisha
Mwajiriwa mpya ambaye ni mwanachama wa PSPF, atastahili kupata mkopo huu baada ya kuchangia kwa kipindi cha miezi isiyopungua sita (6) tu.
Mkopo huu unalenga kumwezesha mwanachama kumudu gharama kama kulipa kodi ya nyumba, kununua samani za ndani, kugharamia ndoa na harusi, kununua chombo cha usafiri n.k. Mwanachama anaweza kukopa hadi mishahara ya miezi mitatu (3).
Wazo zuri lkn kwa sasa mwache kwanza ajifunze kusave uko mbele ndo aje ingia kwenye mikopo kwasasa ngoja ajibane bane itamsaidia
Ninayo my dearUna pesa ya kula kwa mwezi huu?