uzeebusara
JF-Expert Member
- Apr 15, 2013
- 657
- 514
Je kwa nini arudie mtihani? Ninavyojua, ili kuendelea na Elimu ya juu inahitaji ufaulu wa masomo matatu yanayounda mchepuo. Au je, kanuni zimebadikia siku hizi. Nasema hivyo kwa kuwa kuna watu walifeli GS na BAM, ila walifaulu vizuri masomo ya msingi kwa principla pass, na sasa wapo vyuo vikuu. Hata kama hakufaulu Kidato cha Sita, ufaulu wa Kidato cha Nne, hususani hesabu, unazingatiwa.
Naomba ufafanuzi hapo, ili nijue pa kuanzia kukushauri.
Asante mkuu kwa maswali yako. Kwa suala la kanuni hata mimi binafsi Sijui kwa sasa kama ni zilizile tulizotumia miaka hiyo ya zamani au la. Pili huyu mdogo wangu ktk masomo yake ya principles kapata flat Ds kwenye PCB. Nia yake ni asome udaktari wa binadamu ss alienda kwa lecturer mmoja akamshauri afanye tena mitihani hy ya hayo masomo ya BAM na GS, kwa hl hata mimi sijajua nia ya yule mkuu kumwambia studies mitihani hy ni kuwa asafishe cheti na kuongezea nafasi zaidi ya kuchaguliwa au la hl Sijui. Ss kutokana na hali hy bs dogo kaja wangu wangu hataki llt kwanza mpk afanikiwe suala hl na mm binafsi sina ufahamu wa mambo haya nikaona nitupe kwenu kwa hl ni jukwaa la weledi.
Hata kama hajakidhi vigezo vya kusomea shahada, mshauri asome Stashahada. Mshauri aache kudharau (kama anadharau Stashahada). Kuna vyo kadhaa, hususani vya binafsi, vinavyotambulika na kutegemewa na serikali kuandaa wataalamu wa afya.
Amini nakuambia, kurudia mtihani ni uwekezaji wa hatari kuwahi kufikiriwa kufanywa na huyo ndugu yako, na kama atafeli jamii nzima ya watu wanomzunguka watakuwa wamefeli kumshauri vyema (labda agomee ushauri).