Msaada: Watoto hawa wanahitaji ndugu! watu wa Arusha piteni hapa

Msaada: Watoto hawa wanahitaji ndugu! watu wa Arusha piteni hapa

Rene Jr.

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2014
Posts
3,737
Reaction score
2,402
Watoto hawa waliokotwa wakirandaranda na kuomba chakula maeneo ya Chang'ombe. Inasemekana walikuwa wakiishi Arusha, mama yao anaitwa Rehema Sanga, aliugua ugonjwa wa akili akawatelekeza hajulikani aliko, baba yao aliitwa Dean Edward Irwin, ni raia wa Marekani aliyekuwa akiishi na Rehema huko Arusha, alifariki mwaka 2011. Kwa vyovyote vile watoto hawa wazuri wana ndugu, kwa yeyote anayefahamu ndugu wa upande wa mama au wa baba awasiliane na Nyumba ya yatima HONORATA-Chang'ombe +255 759-401-818. Pia kama unaweza kuwatembelea kuwatia moyo na kuwasaidia kwa namna yoyote ile tafadhali wasiliana na namba hiyo.
18314_10153251392667573_1857247732112455802_n.jpg

ANGALIZO: Mijadala ya ajabu na kejeli hazitakiwa kwenye uzi huu, watoto hawa wanahitaji moyo zaidi kuliko lawama kwa wazazi.
 
Aisee!!! Ndugu upande wa mama wajitokeze, au hata wa baba huko US, wakidodosa vizuri watapatikana.
Mwenyezi Mungu awalinde malaika hawa, wawe kwenye mikono salama.
 
Kama baba ni mmarekani basi hao watoto wapelekwe ubalozi wa marekani then itawashughulikia. Marekani haitupi damu yao
 
Watoto hawa waliokotwa wakirandaranda na kuomba chakula maeneo ya Chang'ombe. Inasemekana walikuwa wakiishi Arushwa, mama yao anaitwa Rehema Sanga, aliugua ugonjwa wa akili akawatelekeza hajulikani aliko, baba yao aliitwa Dean Edward Irwin, ni raia wa Marekani aliyekuwa akiishi na Rehema huko Arusha, alifariki mwaka 2011. Kwa vyovyote vile watoto hawa wazuri wana ndugu, kwa yeyote anayefahamu ndugu wa upande wa mama au wa baba awasiliane na Nyumba ya yatima HONORATA-Chang'ombe +255 759-401-818. Pia kama unaweza kuwatembelea kuwatia moyo na kuwasaidia kwa namna yoyote ile tafadhali wasiliana na namba hiyo.
View attachment 229422

ANGALIZO: Mijadala ya ajabu na kejeli hazitakiwa kwenye uzi huu, watoto hawa wanahitaji moyo zaidi kuliko lawama kwa wazazi.
Ninashauri, wewe mwenye kituo, jaribu kuwasiliana na ubalozi wa marekani. watoto hao kama mama yao alikuwa akiitwa Rehema sanga, ni wa kabila la wakinga wa iringa kule kwenye umasikini alikotoa mkanda Betty mkwasa hadi akapata ukuu wa wilaya. inawezekana alikuwa anaishi mjini sio kule lakini kwa ninavyowajua wakinga watoto hao wanaweza wasipate matunzo mazuri kwa ndugu wa kawaida.

wasiliana na ubalozi wa marekani, hao watoto ni wamarekani kwasababu baba yao ni mmarekani, na kama ukiwasiliana nao hata kama wataishi hapa hapa tz lakini ubalozi wa marekani watakuwa wanajua kuwa kulikuwa na raia wao aliyefariki aliyeacha damu yake hapa hivyo wanaweza kuwajibika kwa namna moja au nyingine hata wakiwakana kuwa si raia lakini damu nzito kuliko maji watawasaidia tu.

pili, ubalozi wa marekani unao uwezo wa kutafuta ndugu wa hao watoto walioko marekani, hata kama itaenda polepole lakini Mungu ana njia nyingi, ndugu wa huyo baba yao aliyefariki 2011 wakiwatafuta kwa njia mbalimbali huko marekani wanaweza kupatikana, na wakipatikana hao watoto wanayo haki kuwafahamu ndugu zao wa huko marekani na pengine wanaweza hata kuchukuliwa kwenda marekani. hata kwenye sheria za tz watoto wanayo haki kujua ndugu zao, hivyo peleka ubalozi usaidia kutafuta ndugu zao wa kimarekani, na apohapo tangazo hili la kwenye jamii forums litasaidia ndugu wa kibongo pia wanaweza kupatikana.

vilevile tungasaidia kutangaza kwenye magazeti, ninyi wenye magazeti front page zenu siku zote zisiwe zinajaa ccm na chadema tu, wekeni front page hawa watoto tz nzima itambue kuwa wanatafuta ndugu, lazima watawapata tu na ni watoto wazuri jamani na umri huo hawatakiwi kurandaranda wanatakiwa kwenda shule.

kwasababu wako mikononi mwao, hakikisha yule atakayekuja kujitambulisha kuwa ni ndugu yao na kuwachukua, mnakabidhiana kwa maandishi na mbele ya vyombo vya sheria, kwasababu kuna watu wanaiba watoto, watoto ni dili. kuna mtoto mmoja aliibwa anapoenda shule ana miaka 8 pale kibaha wakampumbaza wakaishi naye kama msukule mwaka mzima kabla ya kukamatwa, hivyo mtu anaweza kuja na kusema tu mimi ndugu yao kumbe anataka kuwafanyia mambo yake.

otherwise, nakupongeza kwa msaada ulioutoa kwa hao watoto, Mungu akubariki.
 
Usiishie hapa tu!! Kuna na wengine wengi huko mitaani wanaranda randa na kuomba chakula pia,watendee kama ulivyo watendea hawa n Mungu atakubariki,isiwe ni kwa sababu tu ya------
 
Ungepata kujua wapi walipokuwa wanakaa arusha na baba yao alikuwa anafanya nini ingesaidia kuanzia hapo.
Ubalozi waweza saidia lkn ni muhimu kujua majina halisi ya huyo raia wa marekani, nahisi at least jina la kwanza linaweza lisiwe sahihi.
 
Usiishie hapa tu!! Kuna na wengine wengi huko mitaani wanaranda randa na kuomba chakula pia,watendee kama ulivyo watendea hawa n Mungu atakubariki,isiwe ni kwa sababu tu ya------

Si ndio maana ana kituo. Wewe umefanya nini?
 
Kama baba ni mmarekani basi hao watoto wapelekwe ubalozi wa marekani then itawashughulikia. Marekani haitupi damu yao
Nakuunga mkono, babayao(rip) aweza kuwa alikuwa na akiba huko amerika
 
Kama baba ni mmarekani basi hao watoto wapelekwe ubalozi wa marekani then itawashughulikia. Marekani haitupi damu yao

Yeah ila nafikiri kwa kuwa wamezaliwa Tanzania watakuwa na uraia wa TZ ila sijui sheria inasemaje upande wa uraia wa baba watu wa sheria watusaidie ila kwa kweli inasikitisha sana!!!
 
anzia ustawi lakini pia nenda ubalozi na jaribu kuona watawasaidiaje, sio kuwa tume mind vile ni wamarekani ila tunaona wanastahili kwani lazima kuna ndugu wenye uwezo wangeweza wachukua au wasaidia na vituo vikaendelea na hawa wa hapa wasiokuwa na ndugu, vituo vinaelemewa mie kuna watoto yatima watatu nimejaribu kuwaombea sana kwenye vituo nimeshindwa kwa kigezo mama ni mzima japo ni mgonjwa pia hayuko vizuri kichwani, baba alikuwa mtu wa Moro na akafia huku hawajui ndugu. Kifupi wanaishi maisha ya kiyatima na kwa rehema tu ya majirani.
 
wakuu nashukuru sana kwa maoni na ushauri. naomba nifafanue tu kuwa mimi siyo mwenye kituo, mimi ni mtu tu niliyeguswa na masahibu yaloiyowafika watoto hawa, kusema kweli kwanza nawashukuru sana kituo cha HONORATA kwa kuwapa hifadhi watoto hawa pamoja na hali ngumu waliyo nayo pale. mimi nashawishika kabisa kuamini kwamba hawa watoto wana ndugu pande zote mbili, na kwa kutangaza hivi ni lazima ndugu watapatikana. upande wa baba tayari kuna msamaria mwema keshajitokeza anaendelea kutrace ndugu wa upande huo, ifahamike tu kuwa kuna bureaucracy nyingi zitakuwa involved hata ndugu wa upande wa baba wakipatikana, lakini for the time being watu wote mnaoguswa na hili itakuwa vizuri mkiendelea kutrace upande wa mama, pia mnaweza kupeleka chochote pale kituoni kuna watoto wengi na uwezo wa kituo ni mdogo.
 
Sasa bureacracy inatokea wapi??
Marekani wana database ya watu wao kuanzia karne ya kumi na ushee cjui, hivyo kama kweli mzazi ni Mmarekani watatrace ndugu kupitia database hiyo then watafanya DNA na kuilingansha na ya watoto ikimatch watatafutiwa utaratibu wa kuwatunza. Wao wana foster care na adoption system so sioni kwa nini wanateseka watoto.
 
Back
Top Bottom