Mkuu hongera kwa wazo zuri
Tatizo ni kuwa mabenki yetu sio rafiki sana na sisi watu wa chini au kati. Kuna benki nishajaribu ila kuna vikwazo ambavyo kiasi chake ni kizungumkuti. Mfano ni dhamana uliyonayo kwani mathalani kwa sasa lori jipya yaani hose na trela la kichina si chini ya mil. 180 hivyo dhamana yako iwe ina cover almost zaidi ya 125%, pili uje katika suala la miamala yako na taasisi husika unayotaka kukopa, tatu uje masuala ya utunzaji wa mapato na matumizi na faida na hasara za mahesabu yako katika biashara. Mimi nilijaribu Equity bank na I and M bank Tz ltd lkn hali ndiyo hiyo.
Ishu ya Rais kuweka agizo la kuzitoa pesa katika mabenki ya kibiashara haya ni bonge la ishu kwani sasa hata wenye mitaji midogo tutaanza kuonekana tuna thamani. Hivyo kama wataka kukopa jipange na baadhi ya mambo hayo niliyokupa dokezo hapo juu
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.