Msaada: Waliofaidi mshahara wa mzee wangu naweza kuwashitaki?

shikulaushinye

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
828
456
Bila kuwachosha mzee wangu alikuwa mtumishi wa serikali akatengenezewa zengwe akaachishwa kibarua tangu mwaka 2008, baada ya serikali ya JPM juzi aliitwa na tume maalumu inayohakiki watumishi hewa, nae aliambiwa ni mtumishi hewa, alionyesha vielelezo vyake akaachiwa huru, kumbe waliomtengenezea zengwe walikuwa wanakula salary kwa jina lake.

SWALI: Je mzee wangu anaweza kushtaki kwa watu kujipatia fedha isivyo halali kutumia jina lake? Pia anaweza kudai fidia kwa usumbufu alioupata wakati yeye si mfanyakazi tena?

Vijana wanasema kama mbwai basi na iwe mbwai.

Kwa sakata hili najua wengi linawagusa hivyo naomba mod asiupeleke uzi huu kule uani.
 
Anawajua waliokuwa wanapokea???

Bado hatujamua kuwatambua lkn ni rahisi, hata km tusipojua jina lake moja kwa moja lkn mgurugenzi na afisa utumishi si wanajua waajiliwa wao? kwa sababu mpaka mzee ameitwa na tume kuhojiwa ina maana wameona aliyekuwa anakula mshahara wake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom