Zipo nyingi ila inategemea na uwezo wa kompyuta na uchumi wako.
1.Adobe Premiere Pro...hii ni kama standard Ya kiofisi ina kila tools zinazohitajika kwa ajili Ya video editing kama vile effects,trimming,audio and video editing tools na exports kwenda kwenye any format or device.
Changamoto Ya software hii ni kwamba inauzwa. Pia, inahitaji some serious memory kwenye compyuta yako kama unafanya kazi kubwa mfano:ku-join clips za video, au kutengeneza video kwa kutumia still images. Pia, inaboreshwa kutokana na graphic card unayotumia. kujifunza Pia kunahitaji muda, hasa kama huna Elimu kabla Ya Adobe softwares.
2. Windows Movie maker...hii ni Ya Microsoft windows, ambayo kuanzia windows 7-10 Itabidi u-download kama separate software via page Ya Microsoft. Hii software ni maarufu kutokana na urahisi wake wa kutumia. Haina vitu vingi, kujifunza ni simple and clear ndani ya siku moja unajikuta unatengeneza clips na export Kwenda kwenye any file format. Pia ni bure.
Kwa sababu hii, changamoto Ya W.movie maker ni kwamba haina tools nyingi, ipo simple sana, so kama ni mtu unayependa control sana kwenye video zako, itakua shida.
3. Aurora Movie Maker (kama nimeitaja sawa lakini tumia Google kwa uhakika)
Hii ipo kati Ya Adobe Pr. na W.movie maker Pia ipo Ya bure na Ya kununua. Nimetumia sana hii baada Ya kupata matatizo na Movie maker kwenye win8. Ipo faster kama ni mtu unayetaka kutengeneza video kutumia clips ndogo ndogo, Pia ina uwezo wa Kuweka effects kama "sharpen" na ina more control Japo sio kama Adobe Pr. Kujifunza Pia ni rahisi na ipo more fluid, unaweza kufungua icon chache au nyingi zaidi
Enjoy!