Msaada wa zawadi ya kumnunulia mwanangu

baiskeli ya miguu mitatu
zipo toy nzuri ambazo sio za umeme
viatu vinavyo toa sauti akikanyaga
mpira..
Umenikumbusha waqt wetu zilikuwepo za mbao wacha kabisa dunia inakwenda kasi sana enzi za filimbi za kigogo zile za mbao utoto raha sana.
 
Sister kama upo nje ya nchi hayo makorokoro (Toys) ukienda duka lolote la vitu vya watoto unakutana nayo, kuanzia Prams, Strollers, Walking rings, nk. Muhimu ni kutafuta section ya makorokoro unayoyataka
Itabidi nimwagize mtu ambae yupo nje ya nchi.
 
Kuna I pad za watoto zakujifundishia kusoma ni nzuri pia,bei yake ni hapo kati ya laki moja na nusu mpaka mbili sio zaidi
na ni imara sana...mwenyezi mungu ampe mapenzi zaidi ya unayompenda na awe mtoto mwema Ameen.....
 
Hivi mkuu umeshindwa nini kupost picha za watoto wa kiafrika badala yake upost za watoto wa kizungu tu?
Ubaguzi umekujaa huna lolote.

Nilichofanya hapo ni kuonesha mfano wa zawadi, na si kingine.

Sasa na wewe unakuja na mengine tena.

Watu wengine bana
 
Kuna I pad za watoto zakujifundishia kusoma ni nzuri pia,bei yake ni hapo kati ya laki moja na nusu mpaka mbili sio zaidi
na ni imara sana...mwenyezi mungu ampe mapenzi zaidi ya unayompenda na awe mtoto mwema Ameen.....
Nazifahamu, zina na Game, Hisabati, Maandishi, jinsi ya kuchora, nk. jumla idadi ya vilivyomo inafika kama 68 hivi
 
Naomba katika hizo zawadi utazo amua kununua mama yake asikose zawadi, maana huwa tunasahau sana..
 
Mpatie upendo wa dhati kwa kuwa naye muda mwingi, cheza, ongea, imba naye na kumtembeza ukimounesha vitu mbalimbali na kazi zake.
 
Nazifahamu, zina na Game, Hisabati, Maandishi, jinsi ya kuchora, nk. jumla idadi ya vilivyomo inafika kama 68 hivi
khaswaaaaaaaaaaaaa .....nzuri sanaa mie watoto napenda sana kuwanunulia inawasaidia kuwatayarisha na shule....
 
Mpatie upendo wa dhati kwa kuwa naye muda mwingi, cheza, ongea, imba naye na kumtembeza ukimounesha vitu mbalimbali na kazi zake.
Nafikiri kuna baadhi ya Watu bado hawajamuelewa mleta uzi, ni hivi:-

Tufanye hayo yote uliyoyataja anamfanyia mtoto wake.

Tuweke pembeni na suala la kumfungulia mtoto wake Akiba kama wadau kadhaaa walivyoshauri.

Turudi kwenye swali lake ambalo linasema,

Je nimnunulie zawadi gani itakayomfaa kwa umri huo na kuendelea?
 
Mmh basi nikajua mwanao anaolewa au kuoa loh! Wazazi mnamambo! Teh! Mwaya kwa umri huo doh! !laabda umnunulie yale matoy magari makubwaaa au ndege aje kuwa lubani! Teh!

Kuzaa raha sana, halafu mtoto anakuja kuwa mtukutu, mzazi lazima aishiwe pumzi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…