Msaada wa ushauri

kibebi

Senior Member
Joined
Feb 22, 2013
Posts
111
Reaction score
267
Hili sijui ni tatizo au lah huwa ninapenda sana kufwatilia umbea wa mjini. kama wakigombana huwa ninapitia comments zote ndipo moyo wangu uridhike. asubuhi lazima nipitie blog zote, global publishers, JF na kwingineko kabla ya kuanza shughuli zangu za kila siku. Nimejaribu kiuacha ninashindwa. Nifanyeje wadau? hii tabia wakati mwingine inanikera kwani ninapoteza muda wa kufanya ishu zingine.
 
weka time limit kwa muda wako.. say may be per day tumia si zaidi ya dk 45 kwa mambo hayo ili uweze kupata muda wa kufanya kazi na kujenga jamii!!
 
mim pia muda wote kwenye computer kupitia blogs zote na kusoma habari.hiyo ni asubuh mpaka jion. uzuri mimi ni boss. natoa maagizo tu kwa simu uku nafatilia habari na kuchat
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…