Jiulize na utafute majibu ya maswali yafuatayo utapata kitu sahihi cha kufanya. Nini kinahitajika( nitauza nini ?), Nitauza wapi ? Wakati gani kinahitajika ? Gharama zake zipoje? Unaweza kulima mchicha ukapata fedha nyingi kuliko zao lolote ila je ulipo unaweza kuuza mchicha ? Je unaweza kuuza mchicha msimu wowote au ni kiangazi tu,kwa kuwa masika kuna mbogamboga nyingi?