h120
JF-Expert Member
- Jan 10, 2012
- 2,543
- 3,354
Habari wanajamvi,
Kuna binti nafahamiana nae, alihitimu diploma ya civil engineering mojawapo ya vyuo vya umma, baada ya kuhitimu, alirudi kwao.
Baada ya muda mrefu kupita nimekuja kuwasiliana nae juzi, katika maongezi na kupashana habari kujuliana hali, nikamuuliza kwa sasa unashuhulika wapi, akajibu alihangaika sana kupata pa kujishikiza ila baadae alikuja kupata sehemu ya kujishikiza kwa wakandarasi, nikampongeza kwa juhudi za kuhangaikia kipato, wakati naendelea kumuuliza maswali kuhusu kampuni yao au hapo anapofanyia kazi, nilipenda kujua nafasi yake hapo, alinieleza wapo watatu, kingine ni kwamba ofisi ilikuwa haijasajiliwa au kwa lugha nyingine haijapata vibali vyote muhimu ili kuendesha shughuli za ukandarasi kwa level husika, baada ya kunieleza hayo nikajua tu kati ya hao wawili yawezekana tu ni mafundi, na wasio na vyeti ndio maana wakashindwa kufanya usajili, na kweli nilimuuliza na hilo ndo lilikuwa jibu, nikauliza vipi usajili, jibu nikapewa upo kwenye process, swali lililonijia nikamuuliza kwa hiyo wanatumia vyeti vyako kusajili kampuni ERB akasema ndio, nikamuuliza je utanufaika vipi na vyeti vyako kutumika hapo, akasema ya kwamba wamempa share ya 10% ya kampuni, nilipata shaka kidogo, binafsi nimeona kama atapigwa na nilimweleza kabisa si sahihi, na nimemwambia nitampelekea ushauri madhubuti pamoja na mwingine kutoka humu jukwaani kwa wadau, uzuri ni kwamba hawajasaini mkataba wowote wa mgawanyo wa mapato, ila amejaza tu zile form za maombi kwa ajili ya kusajili kampuni.
Nakaribisha maoni kutoka kwenu wadau na pia itakuwa namna moja ya kuwafunza na wengine wanaokutana na mambo kama haya.
(Ziada naona binti hajatambua umuhimu wa elimu na vyeti vyake, kwasababu wakati namwonya juu ya kudhulumiwa au kukosa stahiki yake muhimu, alijitetea kwamba hakuona shida sana kuchukua uamuzi huo kwasababu alitaka kujifunza zaidi kazi)
Karibuni.
Sijafahamu kama mada ipo jukwaa sahihi,