Msaada wa ushauri kwa mtoto aliyefeli form two

angekua huku kwetu ningeshauri ajifunze ufundi ujenzi kama hataki kabisa shule ila ni vema akajalibu tena anaweza akafaulu tu
 
Kama uwezo wake ni tiamaji tiamaji, mpeleke chuo cha ufundi kulingana na interest yake. Huko sekondari atapoteza muda wake bure
 
Mtafutie kwa garage makini na yenye vifaa akacheze uku anaweza kuja kua mkali wa mitambo magali badae tafuta zile za maroli na mitambo wabembeleze wamchukue utaniambia nimeona kesi kama iyo dogo sa ivi anapiga hela na anadoma sekondari ya miaka miwili QT kisa kuna mwanga kauona mbele kikwazo shule na ana performance nzur nzur darasan nw wanakua sio awana akili sema mwanga mbele ana aelewi anataka nn ila kikwazo kwake ndo kinatakiwa mana wanakua wazur kwa kutatua kwaio akikutana na kikwazo elimu atapiga kitabu utadhangaa mwenye ila usimpeleke garage bubu
 
Big up sana kwa ushauri
 
Hayo ndiyo mawazo magumu tunayohitaji sisi kama wazazi. Unaweza shangaa hili tu la kurudia shule anaipenda balaa na hatimaye analeta matokeo chanya hadi unashangaa.ila siyo kukata tamaa.
Nimekusoma kiongozi Asante
 
Nami nafikiria kufanya hivyo, Asante kamanda
 
Baada ya kupiga nae stori kiurafiki akaniambia anataka kujifunza udereva japo simuoni sana akiwa na interest na mambo ya magari.
Maisha mazuri (mafanikio) hayapatikani darasani tu. Kuna fursa nyingi za kiuchumi. Mm mwenyew nasoma ila nataka kujiajiri kwenye kilimo, sina mpango wa kuajiriwa hata kidogo
 
Mkuu pole sana huwa inanisikitisha hii kitu. Najua namna gani unaumia kama mzazi; wakati huohuo namuonea huruma kijana anakua ktk mgumu kwa mazingira ya dunia ya sasa. No matter what msogeze hivyo hivyo mpaka kidato cha 4. Kutoka hapo mpeleke kozi za ufundi. Na katika kozi za ufundi asome fani zaidi moja ili kumpa options tofauti na uwanja mpana wa shughuli.
 
Hakunaga mtoto asiye na akili. Ni changamoto ya mazingira na ufuatiliaji wa mzazi na mtoto kuwa responsible kutambuwa wajibu wake.

Kwanza unatakiwa umsute ajue yeye ni mtoto na tabia ya kuwapangia na kuwaletea wazazi kiburi hiyo ni tabia ya kijinga sana.

Anatakiwa afahamu wewe unamtakia mema tu na hakuna namna atafanikiwa katika maisha kama atakudharau wewe kama mzazi.

Tunagepu kubwa sana siku hizi kati ya wazazi walimu na watoto. Watoto wadogo wanataka kujifanya wameshayajua maisha wanataka kujifanyia maamuzi.

Wewe ndie baba yake, usiogope kumnyoosha mtoto, malezi ya kudekezana waachie wazungu, mjengee mazingira kuwa mambo mengine tmyatawezekana mara tu atakapokubali kusimamia ukucha elimu unayotaka ahitimu.

Usiishi nae kama mtu mzima ndugu, wewe ni mzazi na huyo ni mtoto. Elimu ni kitu cha lazima. Atakuja kukushukuru akiwa mtu mzima wa miaka 30+ huko mbeleni siku zijazo. Wangapi utawasikia wanakwambia daaah baba /mama alikuwa mkali sana ila kumbe alikuwa ananisaidia, maana bila yeye, leo hii mimi nisingekuwa hapa.

Akili huwa zinawarudia wakiwa wakubwa kwa sasa hapo ni shetani ndio katawala kichwa chake. Nakuja inbobo nikuhoji vizuri maana nina uchungu sana na hawa watoto wa miaka hii.
 
Yes na Mimi nawaza hivyo
 
Tafuta watu wanaoweza kumshauri vizuri hasa wataalamu wa saikolojia kaka
 
Tunatakaga watu kama nyinyi
 
Kwa staili hii kamwe hatofanikiwa! Trust me!! Fimbo hazijawahi kumfanya mtu akawa ana akili
 
Big up sana mkuu nimekusoma Kwa ushauri.
 
Mkuu ni kweli kuna tatizo la sisi wazazi kudekeza watoto, Ila kwa huyu tangia primary nilikuwa na balance kuwa mkali kwenye masomo pia ukaribu wa kumweleza umuhimu wa shule, sema ndio ana kichwa kizito mbaya, na kwa umri aliofikisha sasa Ukali sana ndio hausaidii kabisa zaidi namtahadharisha majuto baadae Ila ndo akili za kitoto hawaoni future yao itakavyokuwa,. Yaaani shida sana jombaaa, malezi haya!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…