Msaada wa tafsiri ya warning light hii kwenye Suzuki Carry (Kirikuu)

Dafo

Member
Aug 1, 2012
75
69
Wakuu habari za asubuhi,

Tafadhali naomba msaada nilikuwa naendesha Suzuki Carry (kirikuu) lakini ghafla ikawasha hiyo warning light kwenye dashboard. tafadhali naomba kuelewa hiyo taa inamaanisha shida iko eneo gani au shida ni nini kabla sijaenda kwa mafundi wetu?

KIRIKUU WARNING LIGHT.jpg
 
Umejibu swali moja mkuu.
Madhara yake ni yapi hasa?
Inarudishika?
Madhara yapo kwenye mafuta.

Catalytic converter inafanya content ya moshi kuwa Carbon dioxide na maji. Hii inasaidia sana kutochafua mazingira.

Bila Catalytic converter gari yako itakuwa inaemmit Carbon monoxide(CO), Hydrocarbon(HCO) pamoja na Oxygen gas.

Uwepo wa Oxygen sensor baada ya catalytic converter inaweza kusense kwamba kiasi kikubwa cha Oxygen gas kinapita iwapo tu catalytic converter itaondolewa (rejea emission inayotoka bila catalytic converter).

Kitendo cha Oxygen gas nyingi kuwa detected kinatafsiriwa na Control Box (ECU) kwamba mafuta mengi yanaingia kwenye engine hivyo ECU itaforce mafuta yanayokuja kwenye engine yapungue (kwa kupunguza muda wa nozzle kuwa wazi).

Ndio maana gari zingine ukitoa masega lazima iwe na misfire.

Natumai umenielewa.
 
  • Thanks
Reactions: RR
Back
Top Bottom