Mkuu
mbapa,tambua mambo yafuatayo. Mosi,wosia si lazima uwe wa maandishi. Wosia wa maneno waweza kubishaniwa na kuthibitishwa mahakamani. Mashahidi waweza kuwa waliosikia marehemu akitamka jambo hilo.
Pili,mahakama haigawi mali za marehemu. Mahakama humteua Msimamizi na kumsimamia katika kutekeleza majukumu yake kama Msimamizi.
Tatu,taratibu za kuteua Msimamizi wa Mirathi,za kimahakama,zapaswa kufuatwa. Hiyo itatoa nafasi ya kujibiwa kwa hoja zenye ubishani baina ya warithi.
Nne,uhalali wa wosia utategemea masharti yatakiwayo na dini ya marehemu au kabila lake. Yategemea aina ya maisha aliyoyaishi marehemu kama ni ya kidini au ya kimila/kikabila. Kila dini au kabila lina sifa za wosia unavyopasa kuwa.