Mbimbinho
JF-Expert Member
- Aug 1, 2009
- 8,328
- 7,783
Habari zenu wakuu.,
Ninaomba kujua sheria hapa ikoje, nielezee kwa kifupi tu swala lenyewe.
Mzee wangu mimi alinunua kiwanja maeneo ya kibaha, ni kiwanja kilichopimwa kabisa. Yeye aliuziwa kihalali kabisa kwa kuihusisha serikali ya mtaa ule na mtendaji akiwa mmoja wa viongozi waliokuwepo katika mauziano hayo.
Nyaraka zote halali za mauziano mzee wangu anazo.
Sasa tatizo limekuja baada ya aliyekuwa mke/mtalaka wa aliyeuza kiwanja kusema kuwa wakati wa talaka mahakama ilitoa uamuzi kuwa kiwanja kile kiuzwe then huyu mama apate asilimia kadhaa ya pesa ya mauzo., Mtalaka huyo anasema alimwambia aliyekuwa mme wake kuwa wasiuze ili kije baadaye kiwasaidie watoto na wakakubaliana hivyo mbele ya mahakama kuwa kama wameamua hivyo basi mahakama itabariki uamuzi wao.
Lakini baada ya miaka kadhaa huyu mme aliamua kukiuza kiwanja bila kumshirikisha mtalaka wake. Huyu mama mtalaka baada ya kupata taarifa akaja kushtaki kwenye serikali ya mtaa ambako mzee wangu akaitwa kwenye shauri hilo. Yule jamaa (mme mtalaka) aliyeuza kiwanja hapatikani na hajulikani anakoishi. Sasa kwa kuwa wamemkosa wamepitisha shauri kuwa mzee wangu ampe yule mama mtalikwa sh mil 1.75., na kama akishindwa watapiga mnada kiwanja alichonunua mzee. Mzee alinunua kiwanja mil 17.
Wakuu naomba kujua, kulingana na sheria je hawa jamaa wako sahihi? sheria inasemaje hapo maana mzee wangu alinunua kihalali na dokumenti zote muhimu anazo.
Msaada wakuu