Msaada wa nyimbo hizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa nyimbo hizi

Discussion in 'Entertainment' started by Dio, Sep 14, 2012.

 1. Dio

  Dio JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 1,278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mambo vipi wapendwa,
  Natumaini sisi sote ni wazima ninaombi kwa mwenye nyimbo hizi za Tanzania ambazo ni Tazama Ramani utaona nchi nzuri. Na Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote
  Naomba kwa mwenye nazo au sehemu ambayo naweza kwenda na kuzipata.
  Asanteni sana.
   
 2. serio

  serio JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 5,925
  Likes Received: 1,135
  Trophy Points: 280
  katabazi.webnode.com
   
 3. S

  Sangomwile JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2012
  Joined: Aug 17, 2012
  Messages: 3,091
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  TBC utapata hadi video.
   
 4. nyaucho

  nyaucho Member

  #4
  Sep 29, 2012
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13

  Kutoka Michuzi blog Mkuu;
  TAZAMA RAMANI  Tazama ramani utaona nchi nzuri
  Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka,
  Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri,
  Nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzaniaaaaaaaaaa....
  Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
  Utumwa wa nchi, Nyerere
  ameukomesha X2  Chemchem ya furaha amani nipe tumaini,
  Kila mara niwe kwako nikiburudika,
  Nakupenda sana hata nikakusitiri,
  Nitalalamika kukuacha Tanzania.
  Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
  Utumwa wa nchi, Nyerere
  ameukomesha X2


  Nchi yenye azimio lenye tumaini,
  Ndiwe peke yako mwanga wa Watanzania,
  Ninakuthamini hadharani na moyoni,
  Unilinde name nikulinde hata kufa.
  Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
  Utumwa wa nchi, Nyerere
  ameukomesha X2  TANZANIA NAKUPENDA

  Tanzania
  , Tanzaniaaaaaaaaaaaaaa...
  Nakupenda kwa moyo wote
  Nchi yangu Tanzania
  Jina lako ni tamu sana
  Nilalapo nakuota wewe
  Niamkapo ni heri mama we
  Tanzania, Tanzaniaaaaaaaaaaaaaa, Nakupenda kwa moyo wote.  Tanzania Tanzania
  Ninapokwenda safarini
  Kutazama maajabu
  Biashara nayo makazi
  Sitaweza kusahau mimi
  Mambo mema ya kwetu kabisa
  Tanzania Tanzaniaaaaaaaaaaaaaa, Nakupenda kwa moyo wote


  Tanzania Tanzania
  Watu wengi wanakusifu
  Siasa yako na desturi
  Ilituletea uhuru
  Hatuwezi kusahau sisi
  Mambo mema ya kwetu hakika
  Tanzania Tanzaniaaaaaaaaaaaaaaaa, Nakupenda kwa moyo wote


   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,581
  Trophy Points: 280
  Ule wimbo wa Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wangu kwa maoni yangu ndio ulistahili kuwa wimbo wa Taifa una maeno matamu sana ambayo yanakugusa mpaka penyewe kabisa.
   
 6. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,663
  Likes Received: 3,317
  Trophy Points: 280
  Huo wimbo hata mimi naupenda sana.
   
Loading...