Mambo vipi wapendwa,
Natumaini sisi sote ni wazima ninaombi kwa mwenye nyimbo hizi za Tanzania ambazo ni Tazama Ramani utaona nchi nzuri. Na Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote
Naomba kwa mwenye nazo au sehemu ambayo naweza kwenda na kuzipata.
Asanteni sana.
Kutoka Michuzi blog Mkuu;TAZAMA RAMANI
Tazama ramani utaona nchi nzuri
Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka,
Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri,
Nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzaniaaaaaaaaaa....
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere
ameukomesha X2
Chemchem ya furaha amani nipe tumaini,
Kila mara niwe kwako nikiburudika,
Nakupenda sana hata nikakusitiri,
Nitalalamika kukuacha Tanzania.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere
ameukomesha X2
Nchi yenye azimio lenye tumaini,
Ndiwe peke yako mwanga wa Watanzania,
Ninakuthamini hadharani na moyoni,
Unilinde name nikulinde hata kufa.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere
ameukomesha X2
TANZANIA NAKUPENDA
Tanzania, Tanzaniaaaaaaaaaaaaaa...
Nakupenda kwa moyo wote
Nchi yangu Tanzania
Jina lako ni tamu sana
Nilalapo nakuota wewe
Niamkapo ni heri mama we
Tanzania, Tanzaniaaaaaaaaaaaaaa, Nakupenda kwa moyo wote.
Tanzania Tanzania
Ninapokwenda safarini
Kutazama maajabu
Biashara nayo makazi
Sitaweza kusahau mimi
Mambo mema ya kwetu kabisa
Tanzania Tanzaniaaaaaaaaaaaaaa, Nakupenda kwa moyo wote
Tanzania Tanzania
Watu wengi wanakusifu
Siasa yako na desturi
Ilituletea uhuru
Hatuwezi kusahau sisi
Mambo mema ya kwetu hakika
Tanzania Tanzaniaaaaaaaaaaaaaaaa, Nakupenda kwa moyo wote