Naombeni ushauri mwanangu amemaliza form 2 2017 lakin bado hajafanya NECTA form 4 yani baada yakumaliza akurudia form 3 shule nyingine na saivi yupo form 4 sasa shule inadai prem number naipataje.
Hapo Inamaanisha unekariri kidato cha tatu 2018 siyo?
Kama ndiyo huwezi kuwa na prem namba Kwa kuwa wakati huo sekondari hapakua na PREMS.
Sasa naamini ulippkaririshwa ulipata kibali cha kukariri kutoka Kwa afisa elimu mkoa.
Chukua hicho kibali kipeleke shule unayosoma Kwa sasa ili wakiwasilishe necta na hatimaye uweze kusajiliwa kwenye mfumo wa PREMS.
Ndugu zangu Mambo yamebadilika Sana lakini hakuna linaloshindikana.
Kama huko shulen watashindwa kukupa msaada wasiliana na na afisa elimu mkoa wako ili akupe msaada stahiki na ikishindikana basi nenda Kwa kamishna wa elimu Dodoma.
Nadhani nmekusaidia kama hujaelewa uliza. Asante
Kwa uzoefu wangu ni ngumu sana kupata PREM NUMBER hasa alimaliza Mwaka 2017 na ni Mwaka wa zamani sana.
Mwaka jana ilitokea hvo kwa mwanafunzi huku alimaliza kidato cha 2 Mwaka 2016 tulihangaika nae sana aweze kufanya mtihani wa kidato cha 4 hadi mwishoni NECTA walikataa kwa kuwa hakuwa na PREM NUMBER ya Form 2.
Kila la kheri, nawatakia baraka tele kjana aweze kupata PREM NUMBER na kufanya mitihani yake Mwaka huu.