Msaada wa nafasi ya kazi wanajamvi

Regent

JF-Expert Member
Oct 9, 2020
839
1,000
Habari Wanajamvi

mimi ni mhitimu wa chuo, nimemaliza chuo, nimesoma uwalimu level ya degree mpaka sasa ni mwaka wa tatu sijafanikiwa kupata kazi kinachonisikitisha mzazi wangu anaumwa na amedhoofu ananitegea mimi hata pesa ya ku-support matibabu sina.

naomba msaada wenu kupata connection za kazi maana nafikiri kujiajiri sina hata mia mfukoni.

nitafurahi nikipata kazi ya uwalimu wa Geography katika shule...nina uwezo wa kufundisha Geography na Wanafunzi wakafauru vizuri.

Pia nikipata nafasi ya kazi yoyote hata Manual Work naweza ifanya.

Masada wenu niweze kumsaidia mzazi kiafya.
 
digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
4,857
2,000
Pole sana mkuu,Mungu akujalie hitaji la moyo wako,nimewahi kupitia maisha ka hayo yako,hakika najua jinsi unapata maumivu ya moyo

Naimani humu kuna wadau wenye nafasi tofauti watakusaidia,pili tofauti na geography unafundisha somo gani jingine? ni bora nalo ungeliweka hapa
 
Asante Sana
History Pia
 
Ukitu

Senior Member
Jun 14, 2016
111
225
Pole sana
search insta , ajira_biashara_michezo
huwa wanapost matangazo mengi ya kazi hasa ualimu
Natumaini utafanikiwa
 
Bakariforever

JF-Expert Member
Aug 30, 2017
409
500
Kama upo kwenye WhatsApp tuma PM namba yako nimwambie mtu akuunganishe kwenye group la walimu wa WhatsApp kila siku wanatuma matangazo ya shule wanahitaji walimu tena wiki iliyopita kulikuwa na shule inahitaji walimu wa geograph sema ndiyo hivyo.
 
Asante ngoja niweke WhatsApp GB maana simu sioyangu inawhatsApp ya mwenye simu
 
Regent

JF-Expert Member
Oct 9, 2020
839
1,000
Hayo ni mapito kaka, Mungu akusaidie bro. Nakuombea sanaaaa, hata mimi napitia hali kama yako na nilikuja humu kuomba msaada nashukuru waungwana walinipa msaada wa mawazo na kuna waliokuja PM kunisaidia mawazo bado nipo naparangana na namna ya kujinasua bt hali ni ngumu kweli kweli. Nimekuwa mtu wa kula mlo mmoja(nilikuwaga nasikia tu)

Mkuu tahadhali kwa wanaokuja PM, 90% ni mataperi, trust me. Labda kama ni kwangu tu maana kila mtu huwa na ukweli wake.

Binafsi walikuja wengi wawili tulishindwana kwani kazi walizonipa zilihitaji walau niwe hata na 150k+, lakin wote waliobaki walikuwa wananiomba hela ili wanisaidie kazi. Imagine mtu anakuomba 300k et aniunganishe kwenye majina ya walimu ambao hawakuripoti kwenye vituo vyao vya kazi kwenye zile ajira 8k. Mimi sina ata mia alafu nikupe 300k tsh kweli?
Najua kwako watakuja kwa gia ya kuweka jina lako kwenye orodha mpya inayoandaliwa ya majina 5000. Wakikuomba hela mkuu kuwa mzito kuelewa. Mungu ni mwema japo kuwa na uhakika ni vzr ila atatupatia hitaji letu.
Niliiamn jamii forum nilipokuwa nasoma ushuhuda wa waliofanikiwa kupitia jamii forum but saiz nahisi IMEVAMIWA NA WATU WABAYA NA NGUMU KUWAJUA.

Olo ze besiti mkuu🙏🙏
Nimekuelewa Mkuu
 
Bakariforever

JF-Expert Member
Aug 30, 2017
409
500
Habari Wanajamvi

mimi ni mhitimu wa chuo, nimemaliza chuo, nimesoma uwalimu level ya degree mpaka sasa ni mwaka wa tatu sijafanikiwa kupata kazi kinachonisikitisha mzazi wangu anaumwa na amedhoofu ananitegea mimi hata pesa ya ku-support matibabu sina.

naomba msaada wenu kupata connection za kazi maana nafikiri kujiajiri sina hata mia mfukoni.

nitafurahi nikipata kazi ya uwalimu wa Geography katika shule...nina uwezo wa kufundisha Geography na Wanafunzi wakafauru vizuri.

Pia nikipata nafasi ya kazi yoyote hata Manual Work naweza ifanya.

Masada wenu niweze kumsaidia mzazi kiafya.

THE RIGHT FUTURE CONSULTANCY ORGANIZATION (RIFCO)

INATANGAZA NAFASI ZA UALIMU KWA AJILI YA AFRICANA SECONDARY SCHOOL KAMA IFUATAVYO;-

1. Mathematics nafasi 3
2. Physics nafasi 3
3. Chemistry nafasi 3
4. Biology nafasi 3
5. Geography nafasi 3
6. History nafasi 3
7. English nafasi 3
8. Kiswahili nafasi 3
9. Literature in English nafasi 3
10. Commerce nafasi 3
11. Book Keeping nafasi 3

MWENYE SIFA, AFIKE OFISI ZA RIFCO, TEGETA KARIBU NA KIBO COMPLEX KUANZIA TAREHE 13-15/01/2021

MUDA NI KUANZIA SAA 2:00 ASUBUHI

CONTACT: 0756 888896; 0688 365 415
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom