Msaada wa Muundo wa Barua Ya Posa

View attachment 77344 Salams Wana JF wenzangu!

Kama mnavyo jua changamoto za maisha zimetufanya tuwe mbali na familia zetu, hivyo yanapo kuja mambo muhimu ambayo yanahitaji usaidizi wa kifamilia imekuwa shida sana kwa vijana wengi.... Mimi ni kiwa kama kijana ambaye nahitaji kuwa na mwenza wangu wa maisha nimepitia katika kipindi kigumu sana hasa cha kupata watu wakaribu ambao watanisaidia kufanikisha jambo ili..

Nahitaji kupeleka barua ya posa kwa wazazi wa mchumba wangu, tatizo nililokumbana nalo ni watu wakaribu yangu ambao wanaona ili swala kama vile ni kubwa mna, Kabila langu ni mchaga mila na desturi zetu zinatofautiana na baadhi ya makabila ya hapa Tanzania hasa kwenye swala la kuposa binti.

Mila zetu ni kwamba unatafuta wazee watatu mnawatuma kwenda kwa wazazi wa binti wakiwa na Soda au Mbege, na wakifika kule watajieleza wenyewe kwajinsi wanavyo jua na baada ya hapo watajibiwa na wazazi wa binti na kupangiwa mahari na baada ya hapo wanarudi kukujulisha...


Mchumba wangu ni Mnyaturu, kwa mujibu wa mchumba wangu ameambiwa na wazazi wake natakiwa niandike barua ya posa ikiwa na kishika uchumba, ambapo itapelekwa na watu wazima kama wa 3 hivi.. Hapo ndipo palipo nipa mtihani kidogo, kwamba hiyo barua inaandikwa vipi? nimejaribu kuongea na ndugu zangu wameniambia wao hawakupitia utaratibu wa kuandika barua bali walituma watu tu...

Jamani naombeni mnifungue macho kwa maelekezo wa jinsi ya kuandika hiyo barua..


Kwa mujibu wa thread moja humu JF imenipa mwaga kidogo,



Ng'ongoampoku Amenifungua hapa kwa jinsi ya kuiandika barua ya posa, pia ningependa kujua zaidi ya hapa.



Nimepata Sampuli ya barua ya posa inavyo takiwa kuwa toka kwa ndugu Lighondi



Na imani hii thread itakuwa msaada kwangu na kwa wengine wengi tu, Tafadhalini na wakaribisha kwa michago yenu.
 
Back
Top Bottom