Tanganyika1
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 423
- 90
Natanguliza shukurani zangu kwa wajasiria mali na wadau wote wa sekta ya ufugaji. Niseme tu kwamba mmekua na mchango mkubwa katika kusaidia kuinua uchumi wa Watanzania.
Leo hii naomba ushauri wa aina gani ya mbegu ya kuku wa mayai ni bora kwa kuzingatia hali ya hewa ya ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki? Najua hapa kuna wafugaji wenye uzoefu na wataalamu wa kutosha kuhusu kuku.
Aidha nimewahi kufuga kuku aina ya ISA BROWN kutoka pale Interchick Dsm. Moja ya matatizo niliyo kumbana nayo ni pamoja na kuharibika (kuoza) kwa mfumo wa mayai na mayai kabla hayajatagwa.
Nilipouliza kwa mtaalamu akaniambia hilo ni tatizo la kurithi kutoka kwa vizazi vyao na kwamba hakuna dawa ambayo ingeweza kuwaponya.
Hivyo basi kwa yeyote mwenye ufahamu wa mbegu ipi ni bora kwa uzoefu wake atakua amenisaidia sana.
Asanteni.