Msaada wa mawazo

kimbendengu

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2013
Posts
8,424
Reaction score
16,209
Wakuu habari za majukumu ya kila siku niende kwenye ombi langu baada ya kutangazwa matokeo ya kidato cha nne nina ndugu yangu ambae amemaliza shule ya sekondari YUSUFU MAKAMBA jijini dar es salaam ,amepata sifuri .Sasa wadau wa elimu naombeni mawazo yenu tuweze kumsaidia huyu ndugu yetu Asanteni

Sent from my itel S32 using Tapatalk
 
Daaah! Sifuri ina maana hata cheti hapati ni kana kwamba hakuwahi kusoma! Kama mzazi amejaaliwa mashamba mkatie kipande chake akapambane. Kama ndo vipi ajiongeze atafute vibarua vya kujenga au konda wa daladala!
 
Daaah! Sifuri ina maana hata cheti hapati ni kana kwamba hakuwahi kusoma! Kama mzazi amejaaliwa mashamba mkatie kipande chake akapambane. Kama ndo vipi ajiongeze atafute vibarua vya kujenga au konda wa daladala!
Asante kwa mawazo yako

Sent from my itel S32 using Tapatalk
 
kwanza wala usihofu juu ya hilo,huyo ndg yako nakuhakikishia uwezo wa kufauru anao mkubwa ila tu kilichotokea ni kwamba platform aliyokuwepo sio nzuri,hvyo imechangia kufeli kwake.

mimi enzi hizooo wakati nipo shule,nilipata division 0 yaani nilipiga F flat-ukwel nilikata tamaa sikutaman tena kusoma kwa sababu nilijiona sina uwezo darasani.

ila miaka 10 mbele ilinibidi nirudi darasan kwa sababu kile cheti cha form kwa kutokuwa nacho,kilinifanya sehem nying nishindwe kupenya.

nili-reset mwaka mmoja tu nikapata pass kama zote na ma credit,kumbuka nilirudia baada ya miaka 10 nadhan unaweza kuvuta picha hapo.

nachokusihi hiyo kijana kama yupo dar,nitumieni namba zenu PM tuwasiliane ntakuelekeza centre ya kwenda ku-reset,ninachokuhakikishia huyo ndg yako kwa mwaka mmoja tu,atakuleteeni matokeo mazuri saaaana na mtashangaa wenyewe,

kwenye hiyo centre haijawahi kutokea mwanafunzi kukosa hitaji lake kimasomo/walishasoma hapo wanafunz wagumu na walioshindikana kufauru kwenye mashule watokayo ila hapo walifanikiwa niamin hakika nakwambia.

naamini malengo yake ni kufika chuo kikuu baada ya kusoma 5&6 hvyo ndoto yake ataifikia kama utaniamini kwa kumuelekeza akasome hapo paliponitoa kimasomaso kwani hata mimi nilikuwa najisikia kama ajisikiavyo yeye.

natamani niandike vingi ila niishie tu hapo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, kumbuka pia uwezo wa kutunza vitu mbalimbali (memory) tunatofautiana. Kwanza anatakiwa ajue kama mwanafunzi husika anapenda shulee wazazi wasije poteza pesa tuu!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, kumbuka pia uwezo wa kutunza vitu mbalimbali (memory) tunatofautiana. Kwanza anatakiwa ajue kama mwanafunzi husika anapenda shulee wazazi wasije poteza pesa tuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
mimi naamini kabisa huyo mwanafunzi uwezo wa darasani anao,ingekuwa hvyo asingeweza kufauru,tangu darasa la nne,la saba na form two huko.

kinachowafanya wengi wafeli haswa hao division 0 ni pale wanapo_shift kutoka kidato cha pili kwenda cha tatu,walimu wengi huwa hawana mda wa kuwaelekeza ujibuji wa mitihani na kuwapa muongozo kuhusu uandikaji wa essay,

kinachotokea mwanafunzi atakuwa anakimbia mitihani na kutokuipenda shule anaona bora siku ziende tu kwani hata akipewa paper hana cha kujibu.

kwa maana hiyo mwanafunzi anabaki nayo akilini ule ujibuji wa form one na two mpk anaingia necta ya form four mwanafunzi hajui kuandika essay wala topic hazijui.

kwa uzoefu wangu wa kutoka division 0 niliyoipata nilipokuwa school candidate mpk private candidate kuwa na cheti kizuri nashauri huyo mwanafunzi akareset shule ya wasiovaa uniform-atafauru.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yah, Ni kweli mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…