Prince Nadheem
JF-Expert Member
- Feb 25, 2012
- 1,269
- 1,109
Habari za muda huu wanajamii?? Leo nimekuja kuomba namna ya kumshauri huyu rafiki yangu hapa kazini kwetu. Nina rafiki yangu mmoja (girlfriend wa kawaida tu) na pia ni mke wa mtu.
sasa tangu jumatatu namwona hana raha kabisaaaa. Leo tumeenda lunch akaamua kunipa mkasa wa maisha yake.
Alianza kwa kunambia kuwa kabla ya kuolewa na huyu mumewe aliwahi kupata ujauzito akiwa kidato cha nne miaka 15 iliyopita.
Ilikuwa ni mimba ya mwanafunzi mwenzie wa darasa moja. Baada ya mimba kugundulika, mwanaume alikana mimba na kusema hakuwahi hata kuwa na uhusiano nae.
Aliporudi nyumbani familia yao ilifuatilia hilo suala kwa familia ya kijana ila waliishia kutishiwa maisha (wana kijiuwezo kidogo). Hivyo familia ya binti wakabeba jukumu la kulea hadi binti akajifungua mtoto wa kiume.
Dada alirudi shule, akaolewa na mwanaume mwingine aliyechukua dhamana ya kulea mtoto wa dada kama wa kwake na sasa tumeajiriwa sote kwenye idara moja ya serikali Dar.
Sasa shida imekuja kuwa yule mzazi mwenzie na huyu dada kafariki na kwa bahati mbaya hakubahatika kupata mtoto. Hivyo familia ya mwanaume wameanza kuwasumbua familia ya dada kuwa yaishe na wanataka wamchukue mtoto, kwa kifupo they have accepted the responsibility.
Wazazi wa dada wametia ngumu na hao ndg wa mwanaume wamekuwa tubu karaha.
Maswali magumu
1. Anaanzaje kumwambia mtoto kuwa yule sio baba mzazi? (mtoto hajui kama yule sio baba mzaz)
2. Je ile familia ya mwanaume wanayo haki ya kudai mtoto baada ya yote waliofanya? (kuna ushahidi wa serikali za mitaa kiumeni juu ya kilichojiri)
3. Mbona kuja kudai mtoto baada ya wao kupoteza mtoto wao? Maana huyu mtoto wameanza kumpenda kama plan B.
Naombeni msaada wa mawazo kwa maana nilishindwa kumjibu, nimemwambia kesho ntakuja na ushauri kamili.
Cc: Heaven on Earth, lara 1 , Nyani Ngabu , The Boss , Kongosho