Mtaji wa biashara huhusisha UJUZI, UZOEFU, FEDHA, MALI na WATU. Azima Tsh 10,000/- (Elfu 10) au zaidi, tafuta dada au mama yoyote mwenye uwezo wa kupika chapati awe anakupikia chapati kisha uwe unaziuza kwa wateja utakaowapata. Kidogo kidogo mtaji utaanza kuongezeka na kupata mtaji mkubwa wa kuongeza biashara kubwa.