Daddo
JF-Expert Member
- Jan 17, 2013
- 1,435
- 1,025
Kuna dada mmoja tunasoma naye kozi moja hapa Hamburg kwao ni Berlin mbali kidogo na mji huu kwa weliowahi kufika ujerumani wanafahamu miji hii miwili.
kinacho nifanya niombe msaada ni kwamba huyu dada amekuwa ni rafiki yangu wa karibu sana toka mwaka jana. Alikuwa akinifanyia vituko na pengine kunitega kimapenzi lakini hakuwahi kunitamkia kwamba ananitaka kimapenzi.
Mwaka jana mwishoni aliniomba twende nyumbani kwao kutembea nikakubali ila sikujua alikuwa na lengo gani nyuma yake. Basi siku moja tukafunga safari tena ilikuwa ijumaa tukaenda mpaka nyumbani kwao.Kilichonistua ni kwamba nilipofika nilikaribishwa vizuri na familia yake japo baba yake alikuwa hayupo.
Kichwa kilichanganyikiwa baada ya baba yake kurudi nyumbani kutoka alikokuwa ameenda.Yaani ilikuwa kama nachezewa sinema nikiwa usingizini.Ilikiwa hivi, Yule dada alisimama na kuanza kunitambulisha kwanza kila mmoja aliyekuwa pale kwa majina na uhusiano. Ilipofikia wakati wa kunitambulisha kwao sasa ndiyo nikashindwa kuelewa nia yake ninini. Alisema "Vater,das ist ............................. aus Tansania, er ist meinen Freund der ich ihnen schon erzählt" maana yake "baba huyu ni ......................kutoka Tanzania, ni yule boyfriend wangu ambaye nimesha waelezea" basi baba akanikaribisha na zikaendelea stori zingine.
Ilipofika jioni nikamuuliza yule dada kuhusu kurudi chuoni maana nilikiwa sioni dalili za yeye kusema tuondoke, akanijibu eti kutokana na snow iliyopo hawezi kuendesha gari kurudi chuoni kwa kisingizio eti halina tairi maalum kwaswnow.
Kama saa mbili hivi usiku kila mtu akawa anaingia chumbani kwake cha kushangaza yule dada akanikaribisha chumbani kwake. Nilisita ila badaye nikakubali kwenda mle na chumba chake kilikuwa kinaangaliana na chumba cha dada yake.Basi tulipofika ikabidi nihoji kuhusu swala hilo akaniambia amenifanyia suprise.Nilibaki kigugumizi ila nikamuomba tuondoke kwani nilikuwa sikotayari kwa kile alichokifanya.Dada yule akasema hawezi kuondoka basi mimi nikamwambia ngoja niondoke maana nilishaona dalili zisizo za kawaida pale.Yule dada akalazimisha na baadaye ikawa kama mgogoro fulani hivi mpaka dada yake akasikia. Basi nikatoka nje na kwenda kwenye kituo cha mabasi kusubiri pale, baada ya dakika kama nne hivi likaja gari flani aina VW na kusimama mbele ya kituo cha basi. Akashuka dada mmoja ambaye nilimuona muda si mrefu akanifuata pale nilipo. Alikuwa ni dada yake na rafiki yangu yule.Alikuja akaniuliza kwa nini nimeamua kuondoka nikamwambia ninakazi ya kufanya chuoni na zaidi ni kwamba mimi na mdogo wake hatukukubaliana kulala Berlin.
Basi yule dada akaniambia nipande kwenye gari nikamuuliza ananipeleka wapi akasema chuoni kwetu. Nilipopanda akaniambia hatuendi chuoni anataka kunipeleka kwa mdogo wake maana amemuacha analia eti nimemwaibisha kwenye familia.Basi nikamtishia kupiga simu polisi ikabidi abadili mawazo alichofanya akanipeleka hotel moja pale akanichukulia chumba nikalala pale. Usiku nikapokea sms kutoka kwake ananiambia kesho nisiondoke bila kuonana naye. Basi kesho yake akaja tukasalimiana then nikamwambia mimi nataka kuondoka but akaniambia mdogo wake hana amani kwa kile nilichomfanyia.
Basi jtatu yake yule rafiki yangu alikuja kama kawaida kwenye kipindi ila siku nzima hatukuweza kuongea na wala alikuwa hataki ata kuniangalia usoni. Ikapita wiki nzima tumechuniana ila siku moja nikamkuta kwenye restaurant nikampa hi akajibu tena kwa majibu ya mkato basi nikajua alisha kasirika ikabidi namimi niwe namchunia tu.
Wiki iliyopita nikiwa kwenye michezo baada ya kumaliza kucheza mpira na washikaji tukapita sehemu flani ambapo wengine walikuwa wakicheza Tennis. Ghafla nikasikia sauti inaita jina langu, kugeuka nikamuona dada mmoja anakuja nyuma yetu akaniomba tuongee. Yule dada akaniambia nahitajika sehemu flani na rafiki yangu yule wa kike tuliyechuniana basi nikaenda pale.Cha kwanza kuniuliza alisema nimwambie ukweli wangu kwanini namfanyia vile. Nikamwambia wala sina tatizo naye. Akaniuliza kama kunakitu ambacho sikipendi kwake au kuna kitu gani kinachonipa wasiwasi kwake.Ikabidi nimtolee uvivu nikamwambia kwamba mimi na yeye ni marafiki ila hatujawahi kuongelea kuhusu swala la mapenzi ndiyo maana sikutaka kulala kwake maana nilijua ningeweza kushawishika kufanya ngono. Basi ikabidi awe muwazi kwamba ananipenda na asingependa kiona namtesa. Nikamwambia basi kama ni hivo anisubiri nitampa jibu.Ukweli ni kwamba mimi siko so interested sana na wazungu na katika maisha yangu sijawahi kufikiria kuwa na demu wa kizungu kwa kuwa kwanza hawanivutii sana kama madem wa kibongo hasa wale wenye sura natural ukiachana na hawa wa kujichubua.
Baada ya siku tatu nilimuuliza nia yake ya kutaka mahusiano na mimi ninini akaniambia anataka kuishi na mimi nikamwambia tutawezaje kuishi wote ilhali yeye makazi yake ni Ujerumani na mimi ni Tz. Akasema hicho siyo kigezo basi nikamwambia hamna noma tutaona. Baadaye akaniuliza kama nimekubali ombi lake. Nikamwambia ndiyo nimekubali kwa kuamini kwamba nikimwambia hivo itakuwa ni njia moja wapo ya kupunguza usumbufu na maswali. Kumbe hilo lilikuwa kosa kubwa kwangu maana kilichofuata ni kwamba alinirukia na kuanza kudendeka kitu ambacho kilinistua tena.
Kesho yake akaniambia tutoke twende nikamhakikishie kwamba kweli nimekubali ombi lake nikatia ngumu nikamwambia kwetu huwezi kufanya mapenzi na msichana kabla ya kufanya blood test kitu ambacho ni uongo kwa kuamini kwamba huenda angeweza kuogopa na kusitisha mpango wake. Kumbe ilikuwa kama na twanga maji kwenye kinu bana,demu akaniambia asi twende kwenye hospital ya kiraia tukafanye hiyo test na baadaye tuendelee na mambo yetu.
Nikawa sina ujanja ila kwa kuwa nilipoondoka Tz nilikuwa nimeshapima na sijawahi kudo na mtu nikawa sina wasiwasi tukaenda kupima. Kweli keshokutwa yake tulichukua majibu na yalikuwa poa tu sasa hapa nikawa natafuta ujanja tena ila nikakosa. Wikend yake dem akasema haendi nyumbani atabaki chuoni kitu ambacho siyo kawaida kwake. Alivo baki pale muda wote alikuwa chumbani kwangu kwakuwa jamaa tuliyekuwa tunaishi naye alikuwa nyumbani kwao. Basi wikend nzima ikaisha kwa kuvunja amri ya sita na yule dada ila nikagundua kwamba alikuwa na wakati mgumu kwani alikuwa hajawahi kukutana na mwanaume na ndiyo kisa cha yeye kuwa na hamu ya kuingia kwenye ulimwengu huo wa zinaa.
Sasa jamani swala langu ni kwamba ukweli huyu demu sinampango wa kumchumbia wa kumuoa na kibaya zaidi ni kwamba nawachukia wajerumani kuliko watu wengine hapa duniani kutokana na historia yao mbaya lakini ajabu huyu dada amenikomalia na anataka likizo ijayo nije naye Tz angalau apaone nyumbani na mimi nilikuwa najipa moyo kwamba haya mapenzi yataishia huku maana nikisha maliza kozi hata kuwa na uwezo wa kunipata tena nikisharudi Tz sasa je nifanyeje ili demu asipate upenyo wa kuja Tz au nimuache nikiwa bado niko huku na nitafanyeje ili niweze kumuacha?