Msaada wa magonjwa ya ngono na UTI

project planner

JF-Expert Member
Jul 8, 2019
1,166
1,533
Wakuuu naomba msaada nimekuwa nikipata discharge kwenye penzi nyeupe na mbaya zaidi mke wangu naye amekuwa akipata discharge nyeupe kama maziwa mgando yenye harufu.

Tulienda duka la dawa mke wangu akapewa azuma na tenedazole na mimi nikapewa azuma ila tulipata unafuu kidogo ila baada ya wiki ugonjwa ukarudi. Tukaenda tena tukachoma sindano moja moja kila mtu za power safe tukapata unafuu tena kama wiki shida ikarudi tena juzi tumeenda tena tumechomwa sindano mbili mbili kila mmoja juzi moja moja na jana moja moja.

Naomba msaada nitumie na dawa gani hii shida iishe?
 
Mtu yeyote yule aliyeelimika ni lazima anafahamu magonjwa yanagunduliwa maabara baada ya daktari kukuandikia vipimo.

Majibu ya vipimo unarudi nayo kwa daktari na daktari ndio anakueleza tatizo ni nini hapo ndio anaweza kukupa Tiba then unakwenda pharmacy.

Halafu utashangaa kuambiwa mtu kama huyu naye ana degree!
 
Mkuu, Azuma hapo hamna kitu si UTI? Ghono usitumie tablets hapo ni sindano tu bro.
 
Umeruhusu miili yenu iwe ni majaribio ya wauza maduka ya madawa?

Gharama unazotumia kununua dawa na kulipia sindano kwanini msingeenda hospitali pamoja mkafanyiwa vipimo kwa kina na kupewa suluhisho la kudumu?

By the way hiyo unayoiita nafuu na kurudi tena kwa maradhi kunapaswa kukufikirisheni pia. Kuna uwezekano hiyo nafuu ikawa ni kupona kabisa ila mnaishia kujitibu nyie wenyewe tu na pengine kuna mwingine mbali yenu (mchepuko) ambae hajatibiwa hivyo kuendelea kurudisha maradhi ndani baada ya kukutana na mmoja wenu (mwenye mchepuko wake).
 
Wakuuu naomba msaada nimekuwa nikipata discharge kwenye penzi nyeupe na mbaya zaidi mke wangu naye amekuwa akipata discharge nyeupe kama maziwa mgando yenye harufu.

Tulienda duka la dawa mke wangu akapewa azuma na tenedazole na mimi nikapewa azuma ila tulipata unafuu kidogo ila baada ya wiki ugonjwa ukarudi. Tukaenda tena tukachoma sindano moja moja kila mtu za power safe tukapata unafuu tena kama wiki shida ikarudi tena juzi tumeenda tena tumechomwa sindano mbili mbili kila mmoja juzi moja moja na jana moja moja.

Naomba msaada nitumie na dawa gani hii shida iishe?
Umeanzia njiani?

Je Wewe ni mchepukaji?

Kati ya wewe na mke wako dalili zilianza kwa nan?
 
Wakuuu naomba msaada nimekuwa nikipata discharge kwenye penzi nyeupe na mbaya zaidi mke wangu naye amekuwa akipata discharge nyeupe kama maziwa mgando yenye harufu.

Tulienda duka la dawa mke wangu akapewa azuma na tenedazole na mimi nikapewa azuma ila tulipata unafuu kidogo ila baada ya wiki ugonjwa ukarudi. Tukaenda tena tukachoma sindano moja moja kila mtu za power safe tukapata unafuu tena kama wiki shida ikarudi tena juzi tumeenda tena tumechomwa sindano mbili mbili kila mmoja juzi moja moja na jana moja moja.

Naomba msaada nitumie na dawa gani hii shida iishe?
MUWASHO NA KUTOKWA NA MAJIAMJI UKENI Vaginal Discharge.jpg

KUTOKWA NA MAJIMAJI, MUWASHO UKENI (VAGINAL DISCHARGE)
NI tatizo linalowapata zaidi wanawake walio katika umri wa kuzaa ingawa katika hali isiyo ya kawaida inaweza kuwatokea watoto ambao hawajavunja ungo au wanawake watu wazima waliofikia ukomo wa kuzaa ‘menopause’. Tatizo linaweza kuambukizwa kwa njia ya ngono au likatokea tu kama fangasi.
Uchunguzi wa ugonjwa wa dalili hizi hauhusiani na maambukizi ya njia ya mkojo au U.T.I. Ugonjwa umegawanyika katika makundi matano kama ifuatavyo;
Kwanza ni kutokwa na uchafu mwepesi na muwasho ukeni wenye harufu kama shombo ya samaki ‘Bacterial vaginosis’. Pili ni kutokwa na majimaji ukeni na muwasho mkali ukeni hasa sehemu ya nje ya uke na ukijisafisha na maji ya moto unapata nafuu. Ugonjwa huu unaitwa ‘Trichomoniasis’.
Tatu ni kutokwa na usaha ukeni ‘Gonorrhea’ au ‘Gono’. Nne ni kutokwa na majimaji mazito ukeni yasiyo na harufu wala muwasho ila yanakera yakiambatana na maumivu chini ya tumbo. Ugonjwa huu unaitwa ‘Chlamydia’. Na mwisho ni kutokwa na uchafu mzito ukeni wenye muwasho ambao kitaalam ugonjwa huu unaitwa ‘Vaginal Candidiasis’.
Takribani magonjwa yote hayo huambukizwa kwa njia ya ngono isipokuwa fangasi ambayo hutokea kutokana na mabadiliko ya mazingira ya uke na hali ya mwili kwa jumla.
Kwa hiyo hapa tutaanza kuyachambua magonjwa haya yenye dalili za aina moja. Kwa jumla magonjwa haya ni sugu na hata tiba zake hutofautiana. Unaweza kudhani kwamba tatizo la kutokwa na uchafu ukeni halikuishi kumbe unaweza kutibiwa ugonjwa ambao siyo au kumbe una ugonjwa zaidi ya mmoja kwa hiyo suala la muhimu ni kuwaona madaktari kwa uchunguzi wa kina ili kujua una aina gani ya ugonjwa kati ya haya na upate tiba sahihi.
BACTERIAL VAGINOSIS
Ugonjwa huu kwa jina lingine unaitwa ‘Vaginitis’, mwanamke hutokwa na uchafu mweupe ukeni wenye harufu ya shombo la samaki ‘fishy odor’. Kwa kawaida mazingira ya ukeni ni tindikali, lakini katika hali hii mazingira hayo huwa Alkali na katika vipimo vya maabara kuna aina ya chembechembe ziitwazo ‘clue cells’ huwa zinaonekana.
JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA
Tatizo hili hutokea sana kwa wanawake wengi wenye hali ya kutokwa na majimaji ukeni. Katika hatua za awali, takribani asilimia hamsini ya wanawake wenye tatizo hili hawaoneshi dalili, ‘Asymptomatic’.
Ugonjwa huu ni matokeo ya mabadiliko ukeni, ‘Changes of Vaginal Bacterial Flora’ ambapo bakteria wakazi ‘Lactobacilli’ hutoweka ambao ni walinzi hivyo husababisha pia tindikali hapo kutoweka na aina nyingine ya bakteria kuanza kuzaliwa.
Bakteria hawa wapo wengi kama vile ‘Gardenella Vaginalis’, ‘Ureaplasma’, ‘Mycoplasma’ na wengineo. Kutokea shombo la samaki husababishwa na uwepo wa kundi la bakteria waitwao ‘Anaerobic’.
Ugonjwa huu wa ‘Bacterial Vaginosis’ husababishwa na mwanamke kushiriki ngono na mwanaume zaidi ya mmoja, kufanya ngono na mwanaume mpya au mpenzi mpya, kusafisha sana uke ‘Vaginal douching’ na kubadilika kwa mazingira ya ukeni. Kwa hiyo yote, baadhi au mojawapo ya vyanzo hivyo vinaweza kukuathiri cha msingi ni ukafanyiwe uchunguzi hospitali kuthibitisha ugonjwa.
KINGA YA UGONJWA
Kujiepusha na ngono, epuka kusafisha uke sana na kutumia kemikali zitakazokusumbua ukeni, ukitibiwa hakikisha na mpenzi wako anatibiwa au unafanyiwa uchunguzi wa kina. Ugonjwa huu unafanana sana na ugonjwa wa Trikomonia ambao tutauona, kusinyaa kwa uke na tatizo linaloambatana na muwasho mkali wa ukeni.
MADHARA
Mama mjamzito mwenye tatizo ana athari za kupata uchungu mapema kabla ya mtoto kukomaa ‘Preterm labor’, chupa ya uzazi kupasuka kabla ya mtoto kukomaa na mimba changa kutoka.
USHAURI
Tatizo hili kwa mwanamke au mjamzito au la, hutibiwa hospitali baada ya uchunguzi wa kina wa kuchunguza majimaji ya ukeni.
TRICHOMONIASIS
Ugonjwa wa Trikomonia husababishwa na vimelea viitwavyo ‘Trichomonas Vaginalis’. Huambatana na kutokwa na majimaji mepesi sana ukeni, yapo kama usaha yaani ya njano, yana harufu mbaya ambayo hata mtu wa pembeni uhisi.
JINSI UGONJWA UNAVYOTOKEA
Ugonjwa huu huonesha dalili za moja kwa moja kwa mgonjwa. Wanawake wengi wenye tatizo la kutokwa na majimaji ukeni na muwasho ndani ya uke huwa na tatizo hili. Ugonjwa huu kwa asilimia kubwa huenezwa kwa ngono. Mwanaume akiupata hulalamika kuwashwa uume mara baada ya ngono na baada ya muda muwasho hutoweka wenyewe. Hadi ugonjwa kujitokeza tangu ulipofanya ngono ni siku nne hadi 28.
DALILI ZA UGONJWA
Kama tulivyoona hapo mwanzo ni kutokwa na majimaji mepesi ya njano na yenye harufu mbaya ukeni, kuhisi kama joto ukeni, muwasho ukeni kwa ndani na kuwa na hamu au raha ya kujikuna ukeni kwa ndani, maumivu wakati kukojoa mkojo au moto kwenye njia ya mkojo, kwenda haja ndogo mara kwa mara, maumivu wakati wa kujamiiana, kutokwa na damu baada ya ngono.
Pamoja na uchafu kuwa na rangi ya njano kiasi, lakini asilimia kubwa ya hayo majimaji huwa ya kijani na harufu mbaya. Mwanamke akichunguzwa ukeni huwa na makovu ya kujikuna au sehemu za ukeni huwa nyeusi sana.
Ugonjwa huu hufanana kwa karibu na ugonjwa wa ‘Bacterial Vaginosis’ kusinyaa uke na kuharibika kwa ngozi ya ukeni.
MADHARA
Ugonjwa huu husababisha vidonda vikubwa visivyopona haraka ukeni, kuharibika shingo ya kizazi na hatari ya saratani ‘Cervical Neoplasia’, mirija ya uzazi inaweza kuziba na kusababisha ugumba.
USHAURI
Wahi hospitali kwa uchunguzi muone daktari bingwa wa kina mama ambapo vipimo vya ukeni vitafanyika.
UGONJWA WA KISONONO
Ugonjwa huu huitwa ‘Gonorrhoea’ au Gono kama wengi walivyozoea kuita. Athari kubwa za ugonjwa huu hujionesha kwenye njia ya mkojo.
JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA
Ugonjwa husababishwa na bakteria aitwaye ‘Neisseria Gonorrhoea’ kitaalam maarufu kama ’Gram-Negative Diplococcus’ ambapo hukaa zaidi kwenye njia ya mkojo, mdomo wa kizazi, kwenye njia ya haja kubwa au kinywani.
Bakteria hushambulia kizazi hasa mirija ya uzazi na kusababisha tatizo la mirija liitwalo ‘Salpingitis’.
Mkuu ninakushauri uende kupima hospitali katika maabara ili tupate kujuwa unayo maradhi gani ya UTI Sugu yasiyosikia dawa za hospitali. Na hapo ukisha pata majibu nione mimi ili nipate kukutibia kwa dawa zangu ili uweze kupona maradhi yako uguwa pole.
 
Si hamtaki kwenda hospital basi sawa kuna kitu mnakitafuta mtakipata...
 
Back
Top Bottom