Mimi ni mwenyeji wa lugha ya kiingereza, lakini kiswahili bado nakijifunza. Kwa hiyo, naomba unisamehe kwa makosa yo yote yakiwepo.
Swali lako ni zuri sana. Hata wale ambao wameongea kiingereza tangu utoto wanakosea matumizi mazuri ya hilo neno. Kwanza, nionyeshe mifano mbalimbali:
"Do not disturb me further"
"Usiendelee kunisumbua"
"Her second book further discusses the history of that period"
"Kitabu chake cha pili kinazungumzia zaidi historia ya kipindi kile"
Kwa hiyo tumeona "further" ni neno linalotumika kumaanisha "kuendelea" au "zaidi".
Sasa, ninataka niongeze kitu kingine. Kuna neno lingine linalofanana sana na "further", lakini maana yake ni tofauti kidogo. Neno hilo jipya ninalolisemea ni "farther", ambayo ni ndugu ya neno "far" ambayo ni "mbali". Kwa hiyo, tunaweza kuwaza kwamba maana ya "farther" ni "mbali zaidi" au "mbele ya". Ni muhimu kutumia "farther" pale unapoongelea mambo ya umbali, na "further" unapoongelea mambo mengine.
"The petrol station is farther than the bus stand."
"Kituo cha mafuta yako mbele ya stendi ya mabasi"
"New York is farther from Dar es Salaam than London is."
"New York iko mbali na Dar es Salaam kuliko London"
You are welcome to ask any questions.
Sent using
Jamii Forums mobile app