Msaada wa kupatiwa kazi/nafasi ya kujitolea

Kamanda wa Kweli

JF-Expert Member
Jul 13, 2014
1,448
835
Wakuu Salaam!

Mimi ni kijana mwenye shahada ya biashara katika uhasibu. Naandika ujumbe huu,kuomba msaada wa kazi au kujitolea katika kampuni, taasisi, au mahali po pote ambapo naweza kufanya kazi inayoendana na elimu/uzoefu nilio nao au sifa nilizo nazo.
Baadhi ya sifa nilizo nazo ni; naweza kutumia kompyuta vizuri, najua tally accounting vizuri, Nina uelewa kiasi Wa QuickBooks, Nina mkusanyiko mkubwa Wa maarifa ya kurekodi miamala ya kiuhasibu(bookkeeping), naelewa masuala ya kodi na ukaguzi Wa mahesabu. Nina uzoefu Wa kusimamia hoteli ndogo kwa mwaka mmoja. Pia nina uzoefu Wa kufanya kazi za uhasibu kwa zaidi ya mwaka mmoja. Naweza kufundisha masomo ya biashara hasa sekondari, nimekuwa msimamizi Wa Duka la rejareja kwa mwaka mmoja, hivyo kazi zinazo husu kununua na kuuza pia naweza(hasa za walaji).

Ni kijana muaminifu, huwa nafanya ninachoagizwa, mkakamavu, naam, kwa Neema ya Mungu naamini kuwa atakayeniajiri hatajuta, kama ilivyotokea kwa Yusufu na Potifa mkuu Wa askari kuleMisri zamani zile. Wanasema, asiyefanya kazi, asile chakula. Hivyo wakuu, mpaka nimeamua kundika hapa, Nina uhitaji. Maana naweza kwenda mkoa, ila kule gharama za maisha ndiyo zilko chini, lakini sina mahali pa kuanzia. Maana maisha ya DSM bila cha kufanya, naona karibia yananishinda. Dah...siwezi kulia sana hapa....maana najua wengi tuna changamoto.

Pia, naweza kufanya kazi yoyote halali, ili mradi nipewe mafunzo ya kazi hiyo. Hata kazi za nguvu kama za kubeba zege, nk Niko tayari kufanya. Hizo ni baadhi ya sifa nilizo nazo.

Wakuu, mnisamehe kwa Maelezo yasiyoeleweka. Napatikana Dar es Salaam. Asanteni sana. Be blessed.
 
Kijana upo mkoa gani kama hautajali njoo inbox nikuunganishe mahala
 
Hello,naitwa Irene, Nina miaka 20 nimemaliza form 6 natafuta kazi yoyote mwenye any connection anisaidie na Mungu atamzidishia available 0755245221
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom