minji
JF-Expert Member
- Sep 2, 2016
- 2,751
- 4,946
Wanajamii naamin mu wazima na mmeamka salama. Kama uzi unavyojieleza hapo juu nina dada angu aliolewa kwa imani ya dini kiislamu. Alikaa kwenye ndoa yake kwa muda wa miaka 7 alijaliwa kupata watoto wawili ila alishindwa sababu ndoa yao haikuwa na amani hata kidogo, ilijaa vipigo na mambo mengi ambayo nashindwa kuyaandika.
Mwanamke aliamua kuondoka kama miaka 2 na nusu iliyopita na kuamua kurudi kwao na yule mwanaume aliamua kuoa mke mwingine hiyo haikuwa tabu kwa ndugu yetu sababu aliamua kuondoka kabisa. Sasa shida imekuwa ni moja yule mwanaume hataki kutoa talaka, dada angu anamuomba sana talaka yake yule mwanaume anamwambia atamkomesha hampi talaka.
Sasa tulikuwa tunauliza, je BAKWATA wanaweza toa talaka akipeleka malalamiko yake au mpaka aende mahakamani? Kwa yeyote mwenye uelewa wa hili suala ninaomba atusaidie kuhusu hili naamin humu kuna watu wa aina mbali mbali tutapata muafaka.