Msaada wa kupata talaka kwa imani ya kiislam kwa mwanamke

miaka miwili na nusu bila kushiriki tendo la ndoa si ni TALAKA tayari? anaweza fanya mambo mengine hata kuolewa...
au unamaanisha unattaka msaada wa kugawana mali? waliyochuma?....
Unahakika hashiriki tendo? C ajabu na hasira alizonazo ndo zaidi jamaa c ameoa
 
Wanajamii naamin mu wazima na mmeamka salama. Kama uzi unavyojieleza hapo juu nina dada angu aliolewa kwa imani ya dini kiislamu. Alikaa kwenye ndoa yake kwa muda wa miaka 7 alijaliwa kupata watoto wawili ila alishindwa sababu ndoa yao haikuwa na amani hata kidogo, ilijaa vipigo na mambo mengi ambayo nashindwa kuyaandika.

Mwanamke aliamua kuondoka kama miaka 2 na nusu iliyopita na kuamua kurudi kwao na yule mwanaume aliamua kuoa mke mwingine hiyo haikuwa tabu kwa ndugu yetu sababu aliamua kuondoka kabisa. Sasa shida imekuwa ni moja yule mwanaume hataki kutoa talaka, dada angu anamuomba sana talaka yake yule mwanaume anamwambia atamkomesha hampi talaka.

Sasa tulikuwa tunauliza, je BAKWATA wanaweza toa talaka akipeleka malalamiko yake au mpaka aende mahakamani? Kwa yeyote mwenye uelewa wa hili suala ninaomba atusaidie kuhusu hili naamin humu kuna watu wa aina mbali mbali tutapata muafaka.
Dada Jibu ni ndio. Uislam ni dini pekee iliyokamilika. Suala la ndoa lipo very very open ktk Uislam. Yaani taratibu zipo simple sana, Inshort mwambie afike ofisi za Bakwata zilizopo maeneo yao. Yaani ni suala jepesi mno hukuhitaji kulileta huku.
 
Alibadilishwa dini ili akidhi vigezo vya kuolewa na huyo mwanaume au ni suala lake binafsi? Any way sichangii lolote maana mdada mwenyewe hajitambui . Uache njia,na kweli na uzima uende mahali ambapo hapaonyeshi direct way to the heaven
 
Ni mahakama tu ndio inaweza toa taraka za ndoa haijalishi ni nfoa ya aina gani
 
Ila kidiini kuka zaidi ya miezi mitatu bila kuingiliana na mkeo nitalaka tosha, Sio wake tena aolewe tu kama amepata mwanaume wakumuoa
 
miaka miwili na nusu bila kushiriki tendo la ndoa si ni TALAKA tayari? anaweza fanya mambo mengine hata kuolewa...
au unamaanisha unattaka msaada wa kugawana mali? waliyochuma?....
Ni kweli kabisa miaka miwili bila kukutana wala kutoa huduma kwa mke (matumizi) basi hiyo ni talaka tosha unless kama anataka cheti akaringishe insta kama binti machozi
 
Dada Jibu ni ndio. Uislam ni dini pekee iliyokamilika. Suala la ndoa lipo very very open ktk Uislam. Yaani taratibu zipo simple sana, Inshort mwambie afike ofisi za Bakwata zilizopo maeneo yao. Yaani ni suala jepesi mno hukuhitaji kulileta huku.
(Uislam ni dini pekee iliyokamilika.)MH!! haya bana heri yenu mlio wakamilifu !!!
 
Alibadilishwa dini ili akidhi vigezo vya kuolewa na huyo mwanaume au ni suala lake binafsi? Any way sichangii lolote maana mdada mwenyewe hajitambui . Uache njia,na kweli na uzima uende mahali ambapo hapaonyeshi direct way to the heaven
Usiseme hajitambui alibadili din kwa matakwa yake,na mpk hapo sijasimulia kisa kamili kilichomtoa hapo nimeomba tuu muongozo tuu wa kupata taraka mambo hayaend hivyo mkuu
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom