Msaada wa kupata shule

Msaada wa kupata shule

Neema91

Member
Joined
Jan 5, 2022
Posts
6
Reaction score
1
Habarini za majukumu wapendwa na hongereni kwa kazi.

Mimi nina mtoto wa kike ana umri wa miaka 6 lakini mpka sasa haongei vizuri, ni neno moja moja sana napo ni kwa kujitahidi hivyo hivyo. Amesoma Pre-Middle za mchanganyiko na sasa anajiandaa kwa kuingia darasa la kwanza.

Sasa naomba ushauri ama msaada wa kupata shule nzuri, iwe ya bweni (boarding) kwa shida aliyonayo mwanangu.

Pia nafikiria sana nikimpeleka shule za viziwi nahisi ntampoteza kabisa hata neno moja moja analoongea litapotea kabisa, niko njia panda nashindwa nafanyaje.

Msaada kuna wenye uzoefu ya hivi vitu humu?

AHSANTENI.
 
Kama upo Dar mpeleke shule ipo mtoni watamuangalia na kukushauri.
Kama kuna shule ya day ni bora zaidi sikushauri umpeleke mtoto mdogo hivyo boarding unamtesa

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom