Msaada wa kununua simu

Haya sasa twende kwenye maduka yapi yanauza sim genuine?
Msaada tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili nalo ni muhimu hebu chief tunaomba msaada hapa maana wengi wanasema posta ndo kuna simu original

Sent using Jamii Forums mobile app

samsung wenyewe wanauza simu kwenye mawakala wao, jmall wapo, kkoo uhuru wapo, ukishuka chini gerezani mwendokasi wapo etc sema bao zao zimechangamka kidogo compare na madukani.

cha muhimu zaidi ni warranty, na kujua kama simu ni genuine.

1. hakikisha ukishanunua simu unatuma imei kwenye namba ya samsung kuihakiki kama ina warranty.

utaandika neno REG*imei yako# kwenda 15685

hakikisha una hela kwenye simu kama 500 na sio kifurushi, wanakata kama 150 au 250 hivi.

2. hakikisha genuine kwa kutumia cpu z

unadownload cpu z store, kisha itakuonesha specs, nenda gsmarena halafu compare hizo specs kama zinafanana ni genuine kama hazifanani ujue ni kimeo.

risiti muhimu ukishtukia ina.matatizo urudishe.

pia uangalie model kwa hizo nilizokutajia zikiishiwa na F ndio za kimataifa, simu za korea na marekani husumbua, nenda setting kisha about kuona model.
 
Poa chief japo dar ni mgeni ila nitapajua tuuu asante kwa msaadaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…