Msaada wa kubadilisha majina.

eddy king

JF-Expert Member
Apr 1, 2016
558
1,218
Habarini wanajamvi, naomba kwa wenye kujua hatua za kufata kumsaidia ndg yang moja.... ..
Ni kijana mkubwa sasa amemaliza chuo kikuu mwaka jana. Baba yake alifariki akamuacha akiwa na miaka minne (4) kijijini , akachukuliwa na mjomba wake wakaenda kuishi mjini . Wakati anazaliwa alikua na cheti cha kuzaliwa chenye majina yake vizuri ila baada ya kwenda na mjomba wake alibadilishiwa majina akawa anatumia majina ya mjomba wake , Akasoma shule zote kuanzia msingi mpaka chuo akiwa na majina ambayo ni ya mjomba wake na cheti kingine cha kuzaliwa, Sasa mama yake hataki tena aendelee kutumia majina hayo na sasahiv anataka afanye process za kupata VISA afanyaje ili apate kutumia majina yake tena msada.
 
Hilo linawezekana sana tu sema ishu inakuwa ngumu kubadilisha mpaka vyeti vyote. Duuuh!

Aende mahakamani apewe utaratibu wa kubadilisha majina. Atoe na sababu nzito nzito za kutaka kubadilisha jina.

BTW, sioni mantiki ya yeye kubadilisha majina na ukubwa wote huo. Better ajaribu kuapply cheti kingine cha kuzaliwa kuliko kuchukua process ndefu mpaka kuifanikisha.
Mwacheni atumie majina ya mjomba kma fadhila kwake kwa kumsaidia katika mambo yote hayo.
 
why all the trouble?? Kwa uzoefu wangu mdogo....Ni ngumu kiasi kubadili majina yakaweza kuonekana kwenye nyaraka zako zote muhimu. Kwa mfano kwa vyeti vya taaluma ukishafanya mtihani wa form four jina linakuwa kama fixed fulani hivi. Birth certificate unaweza uka-manouvre ukapata pale RITA ambapo utaweza pia kupata passport na visa etc, pia kwa mwajiri siku yoyote ukihitaji kujulikana vyovyote unaenda kwa wakili unaleta kiapo wanakubadilishia - hii wanafanya sana hata wanawake wanaoolewa. Ngoma ipo kwenye vyeti vya kitaaluma, na kwa hiyo utaishi maisha ya kujieleza kila mara ili watu wasikutuhumu kuwa umefoji!
 
Asante mkuu kwa ushauri wako.
 
Wasiwasi wake upo kwenye visa hapo mkuu, mambo ya cheti na baba au mama na hayo mambo mengine haiwezi kumsumbua kweli? Na ndio kitu hata mimi ilikua namuawazia!!
 
Awaone Wanasheria watamsaidia kumuandalia Deed Poll for change of name(s) Kisha ataipeleka kwa Kamishna/ Msajili wa kumbukumbu na nyaraka kwa ajili ya kupata usajili
 
Mkuu,

Kisheria, kwa mujibu wa Sheria za Tanzania, haja yako inatatuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Viapo (the Oaths (Judicial Proceedings) and Statutory Declarations Act.) Unachotakiwa kufanya ni kuandika nyaraka ya kisheria ambayo inajulikana kama "Deed Poll" ambayo ni nyaraka mahususi yenye kukuwezesha kutimiza hiyo haja yako ya kubadilisha majina. Nyaraka hiyo inapaswa kugongwa muhuri na Kamishna wa Viapo (Wakili, Hakimu, n.k.) kisha unaipeleka kuisajili kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Hati/Nyaraka (The Registration of Document Act ) ambapo kwa hapa Dar es Salaam ni pale Wizara ya Ardhi.

Nafikiri angalau nimekupa mwangaza.

Kaka ...
 
Yes asante sana sana , angalau tumejua nini na wapi pa kuanzia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom