Habari zenu wakubwa
natumaini wote wazima,
tatizo langu nikwamba nimejaribu kuchakachua modem ya huawei e153 sasa umeme ukakatika sasa nimejaribu kuitumia inakataa line zote mpaka ya tigo yenyewe,sasa kuna uzi niliusoma humu jinsi ya ku restore nimetafuta mpaka nimechoka,naombeni msaada kama kuna yeyote anayeweza kunipa somo la ku restore ili irudi kama mwanzo.
Asanteni.
Ikikataa inatoa ujumbe gani?tukusaidie ku google?
Lakini unaweza kwa kuanza kujaribu ku-update firmware ya hiyo modem uone
mtazamaji hata mm natka ni unlock moderm yangu kwa hiyo nasubiri maoni ya wataalam kwenye thread yako.
Kweli kabisa kaa la MotoFanya home work kuna thread hapa inafundisha vizuri jinsi ya ku unlock modem hizo za tigo. lakini usichakachue hiyo modem.
Tumia njia hii hapa JINSI YA KUFLASH MODEM ZA HUAWEI E153 | MPEKUZI ni secure na inafanya vizuri bila kuiathiri modem yako
Kweli kabisa kaa la Moto
Pia kuna member anaitwa calvin power search thread alizoazisha kwenye jukwaa hili . Ila nimeshangaa thread yake juzi juzi naona anaongelea mambo ya cost na pm . teh teh teh teh . Anyway binafsi sio mtaalam sana wa hizi modem lakini ukikwama kabisa tutakusaidia ku google na kukulengesha kwenye suluisho. Majibu yote nyenzo zote zipo google. Ni kuchambua pumba na mchele tu......