Msaada wa kiutumishi (mambo ya Lawson)

KIGHERA

Member
Nov 19, 2010
84
27
Habari Wadau,

niende moja kwa moja kwenye ishu yangu, niliajiriwa kwenye taasisi moja ya serikali miaka ya nyuma then nikapata kazi taasisi nyingine nayo ni ya serikali.

Nafasi niliyopata ilikuwa ni nzuri kidogo nikilinganisha na ile ya awali hivyo ikanilazimu kuacha kazi taasisi ile ya awali na kujiunga na hii mpya na nilifuata taratibu zote za kiutumishi ikiwemo kurudisha mshahara mmoja.

Sasa kimbembe kimeanza kwenye hii taasisi mpya, wao walikuwa hawako LAWSON (mfumo wa malipo wa mshahara wa serikali) ndo wanataka kuingiza wafanyakazi wao LAWSON.

Ishu inayonichanganya ni kwamba wao wanadai miaka niliyotumikia kwenye taasisi ile ya awali haitambuliki, so wameni grade utumishi wangu kwa kipindi nilichofanyia kazi kwenye taasisi hii mpya, jambo ambalo linanirudisha nyuma sana ki daraja. Kwangu naona sio sawa sababu taasisi ya awali nilioanzia nilifanyia kazi miaka mingi na sikubadilisha fani na evidence zote ninazo na nimeendelea kutumia cheque no ile ile ya awali.

Mwenye uelewa wa haya mambo ya utumishi wa umma anisaidie tafadhali.
 
Back
Top Bottom