Msaada: Nakojoa sana muda wa asubuhi na usiku

Nzi Chuma

JF-Expert Member
Jun 21, 2015
468
1,142
Habari wakuu,

Tatizo ni la muda mrefu kidogo.. tangu 2020, ninakojoa sana muda wa asubuhi kabla ya saa 5 nakuwa nishakojoa zaidi ya mara tatu.. na usiku naweza kuamka hata mara 7, mchana huwa si saana lakini kuanzia saa 5 hadi saa 12 jioni nitakojoa si chini ya mara 5.

Hii ni ikiwa nitakunywa maji kawaida, kama nikinywa maji mengi, mfano usiku, ninaweza kukojoa, punde baada ya kukojoa nikaumwa tena na mkojo nikakojoa tena.

Hakuna maumivu yoyote ninayopata wakati wa kukojoa, na hata kama mkojo utapishana dakika moja tu kuniuma tena, nitakojoa mkojo mwingi sana kama mwanzo tu.

Nilishapiga mpaka ultrasound kuangalia figo nikaambiwa ziko sawa..U.T.I nimeambiwa hakuna. Sielewi tatizo hasa ni nini?

Msaada tafadhali.
 
Kama unakunywa maji mengi basi utakojoa mkojo mwingi,

Physiology zinatofautiana.

Mimi binafsi naweza kukojoa hata mara 10 usiku na sina tatizo.

Kama huna sukari wala usiwe na wasiwasi, pia kunywa maji kiasi si lazima kujilazimisha kunywa maji mengi sana.
 
Acha ubishi wewe.
Hujui kila tiba ya ugonjwa inatoke kichwani mwako(Mind)??
Unajua kwanini Jpm aliziwia kutangazwa kwa idadi ya waathirika wa Covid-19??
Ni kwa kuwa alikuwa ni mpumbavu Na COVID19 haikumkopesha ikamgaragaza tarehe 17/ 03/ 21 kama Mrundi mwenzie Nkurunzinza
 
Hii hali mimi ninayo kuanzia miaka ya 90. Nimesha pima vipimo vingi na siku onekana na tatizo lolote.
Katika kufuatilia nilipata wataalamu kama wawili na maelezo yao yalikuwa karibia sawa, walisema chunguza wakati wa joto unapotoka jasho unakua hukojoi sana na pia wakati wa baridi ndio unakojoa sana, kwa sababu wakati wa baridi hutoki jasho.

Mimi wakati wa baridi huenda zaidi ya mara 5 asubuhi.

Matatizo haya si ya wote ni kwa baadhi ya watu.

Ninakunywa sana maji kati ya saa 4 asubuhi mpaka saa 10 jioni, usiku mpaka nikiwa na kiu sana.

Kilicho nisaidia zaidi ni kuikubali hali hii.
 
Back
Top Bottom