MSAADA WA KISHERIA

Newmoney

Member
May 1, 2015
17
45
Habari ya mda huu wadau. Mm ni mfanyakazi katika kampuni moja hapa dar es salaam. Kampuni ninayofanya kazi inafungwa si kwa sababu imefilisika ila ni kutokana na garama za uendeshaji na kodi kua juu.

Kampuni imetoa notice ya mwezi mmoja. Yani tarehe 25/6/2019 walituita wafanyakazi wote wakatuambia kampuni itafungwa tarehe 31/7/2019.

Naomba msaada wa kisheria ni haki zipi nastahili kuzipata. Ukiangalia kua hatukupewa mikataba mipya tangu mkataba ulipoisha April 2018. Aina ya mkataba tuliokua tunapewa ni ya mwaka mmoja mmoja Then tumekuja kupewa mkataba mpya June 2019 ambao si wa mwaka mmoja bali wameandika mkataba unaanza April 2018 till lawfully termination.


Natanguliza shukrani zangu kwenu wadau.
 

bora uhai

Member
Jan 15, 2019
65
125
Muajiri kafanya kitu tunaita termination by retrenchment or operation requirements ambayo inapatikana section 38 in employment and labour relation act 2004 kwa kwaida utaratibu wake upo hivi ambao nitahusisha na ulivyoandika na sheria inaongoza vipi

muajiri anatakiwa atoe notisi kwa kiasi cha wiki mbili haya nakuja kwako sasa "Kampuni imetoa notice ya mwezi mmoja. Yani tarehe 25/6/2019 walituita wafanyakazi wote wakatuambia kampuni itafungwa tarehe 31/7/2019." hapa muajiri yupo sahihi

muajiri anatkiwa kusema wazi sababu za kufanya termination by operation requirement nakuja kwako sasa " Kampuni ninayofanya kazi inafungwa si kwa sababu imefilisika ila ni kutokana na garama za uendeshaji na kodi kua juu" hapa muajiri pia yupo sahihi kwa mujibu wa sheria

Naomba msaada wa kisheria ni haki zipi nastahili kuzipata

1. Utaripwa siku ulizofanya kazi kabla ya termination by operation requirement .......................
2. Kiinua mgongo hii ni 50/50 japo sheria inasema operation requirment hamna kiinua mgongo kiinua mgongo kipo endapo muajiri ndo awe amesitisha mkatba na wewe ila kukiwa na mutual agreement anaweza akailipa na kama akilipa itakuwa hiv mshahara wako wa siku utazidishwa mara saba alafu watazidisha mara miaka uliyokaa kwenye iyo kamopuni
3. Notice pay
4. Likizo pia utalipwa kama hukuchukua hii ni mshahra wa mwezi mmoja

Then tumekuja kupewa mkataba mpya June 2019 ambao si wa mwaka mmoja bali wameandika mkataba unaanza April 2018 till lawfully termination. June 2019 ambao si wa mwaka mmoja bali wameandika mkataba unaanza April 2018

Mkataba ukianza April 2018 unatakiwa kuisha march 31 2019 ukiwa ni wa mwaka kwaiyo kutoka may june na july hii ni tayari automatical renew of the contract hivyo basi wanatakiwa kilipa oustanding months from April 2019 up to march 31 2020

Ukionesha terms of the contract to be terminated ingependeza zaidi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom