Msaada wa Kisheria

Puna

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
2,332
3,781
Wakuu habarini za majukumu.Niende Kwenye hoja ya Msingi ni hivi Kuna mtu alikopa fedha kwangu kwa makubaliano kuwa baada ya miezi mitatu atazirejesha,tuliandikishana serikali ya Kijiji kwa mtendaji wa Kijiji yeye akiwa na shaidi wake nami na shaidi wangu.Baada ya kuandikishana akanikabidhi Hati ya kiwanja chenye nyumba ya chumba kimoja na sebule.Makubaliani yalikuwa mwisho mwezi wa tatu mwezi wa nne kapunguza kidogo baada ya hapo alipata ugonjwa alipopata nafuu kakimbia na kuama kabisa.Hapatikani Kwenye cm na simfahamu hata ndugu yake mmoja.sasa nataka kupauza sheria zinasemaji nifuate taratibu zipi?
Natanguliza shukrani.
 
Nenda mahakamani ukafungue kesi ili aitwe aeleze atalipa lini pamoja na gharama au riba au ni kwanini eneo lisiuzwe ili pesa yako ipatikane.

Naamini pesa unayodia sio kubwa, hivyo nenda mahakama ya mwanzo ambayo hiyo nyumba ipo au mlikofanyia mkataba.

Wala huhitaji wakili. watarecord maelezo yako tu, kisha watam summon accordingly.
 
Shukrani mkuu.
 
Back
Top Bottom