Ndugu, kuna mambo mawili hujafafanua. Umeshtakiwa kesi ya jinai au madai?Kama umeshtakiwa kwa kesi ya jinai kuwa unahusika na huo wizi, basi kisheria unapaswa kushtakiwa wewe na siyo kampuni na kama umeshtakiwa kwa kesi ya madai kwa maana ulipe fidia ya vitu vilivyopotea basi kwa kanuni ya " vicarious liability" unapaswa kushtakiwa wewe na kampuni yako.
kwa mtazamo wangu kama bushi loya, ilivyo andikwa hapo juu ni sawa, ila ujue ukichukua dhamana ya kulinda ni lazima ujue ni nini unalinda kwenye eneo la mteja (kwa maandishi).
Mfano: ni vigumu kuwajibika kwa kuibiwa Kompiuta mpakato ndani ya ofisi wakati mlango hauja vunjwa na vingine kama hivyo....labla kama kuna mpango mahususi wa upekuzi kila mtu akitoka ndani ya ofisi.
Ila ukiachiwa magari..ukakuta limeibiwa saidi mira au spea tairi hiyo inakuhusu
Kwa tahadhari: nivizuri kukagua vizuri unacho kabidhiwa kulinda na kama kuna mapungufu ya wazi yawe kwa maandishi. Hii ni muhimu zaidi kwa mteja mpya ambaye huja jua tabia yake (ya kusingizia?)